Tuhuma ya kutoa hukumu kwamba waislamu na Mashekhi wao wameritadi

  • | Thursday, 3 August, 2017
Tuhuma ya kutoa hukumu kwamba waislamu na Mashekhi wao wameritadi

   Ni wazi kwamba wote wamekuwa wanalengwa kutoka makundi ya kitakfiri, makundi yale yaliyotangaza kuwa yeye pekee yanayozungumza kwa jina la Mwenyezi Mungu, na yeye pekee yanayomiliki funguo za pepo na moto. Wao wanakafirisha kila anayehitilafiana nao, na wanamtuhumu kuwa ameritadi na wanahalalisha kumwua; kwani anazingatiwa kutoka mtazamo wao ni kama kafara itakapowaingiza peponi, na damu, mali, nafsi na wanawake wake halali.
Hakuna dini, madhehebu, taifa wala kundi isipokuwa imepata shari ya makundi hayo ya kikafiri, yaliyotoka mbali na dini ya Uislamu na msamaha wake. Hata waislamu wenyewe hawakusalimika kutoka umwagaji wao wa damu, bali tunaweza kusema kwamba waislamu ni watu walioathirika sana na mashambulizi yao, na mwanzoni mwao ni wanachuoni wa umma ambao makundi yale yanawazingatia kuwa ni wanachuoni wa ukafiri wanaowaunga mkono watawala wadhalimu sawa sawa wakiwa -waarabu au waajemi- waliosimama bega kwa bega mbele ya maslahi za wananchi wa kiislamu, na walioziunga mkono nchi za msalaba zinazoupigana vita Uislamu na dola yake ya kiislamu, walioritadi ambao wanawaiba dini ya watu na wanaowangamiza watu wakiwafuata.
Kujibu tuhuma
Hakika tuhuma ya makundi hayo kwa kila anayehitilafiana nao katika mawazo au rai, ni jambo la hatari sana kwa mujibu ya matokeo yake ya kiufisadi kama kuwakafirisha wengine na kisha kuhalalisha kuaga damu zao, nalo ni jambo linapingana sheria ya Mwenyezi Mungu, kwani istilahi hii inamaanisha kwamba mtu fulani amemshirikisha Mwenyezi Mungu, au amekanusha kuwepo kwake au amemshutumu yeye au Mtume wake, nayo ni tuhuma ambayo haithibitiwi isipokuwa kwa kukiri au kwa shahidi wawili walioona kwa macho yao. Pia yakini haiondoshwi kwa shaka; hivyo haijuzu kumsifu mwislamu wa kweli kuwa ameritadi na amekufuru.


Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.