Maoni ya Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali kuhusu toleo la Al-Shabab "Je Umeridhia"

  • | Tuesday, 8 August, 2017
Maoni ya Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali   kuhusu toleo la Al-Shabab  "Je Umeridhia"

Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali kinaona kwamba toleo la Kundi la Al-Shabab ni hatari sana kwa sababu linaweza kuwaathiri baadhi ya vijana wenye upendeleo wa kidini, jambo ambalo kundi la Al-Shabab linalitumia katika hotuba yake iliyojaa kwa kuonyesha upendo na kufufua kwa vijana wa Waislamu kwa lengo la kushinikiza juu ya vijana hao na kuwajaalia sababu ya kuwasha Fitina katika nchi zao, na kufanya mapinduzi dhidi ya viongozi wao, na kuharibu jamii ya Kenya.
Kituo cha Al-Azhar kinasisitiza umuhimu wa kuwafundisha vijana hatari za misimamo mikali, inayozidi kuathiri maendeleo na usalama, basi makundi yenye misimamo mikali yanatumia watu wasio wa hatia kufanya vitendo vikali kwa ajili ya kuharibu jamii badala ya kuijenga, pia kituo cha Al-Azhar kinasisitiza kwamba kulinda vijana kutoka  mawazo makali ni kama kulinda jamii yote kutoka ugonjwa mbaya unaoweza kuiangamiza kabisa.

Image

 

Vile vile kituo cha Al-Azhar kinaashiria kwamba mfululizo wa matoleo ya makundi ya kigaidi na wenye misimamo mikali kama vile kundi la Daesh (ISIS), Boko Haram, Al-Shabab na makundi mengineo ni dalili ya kuwa silaha ya habari na matoleo yanayotangazwa na makundi hayo kwa ajili ya kuwashawishi vijana ndiyo silaha isiyopungua katika hatari yake na mabomu au makombora, ambapo vyombo vya habari ni chanzo kubwa kwa vizazi na chanzo pana kwa mataifa ambao hupata maelezo yao na kutegemea juu ya maelezo hayo kuunda ititkadi, fikira, misimamo na maamuzi yao ya baadaye, aidha vyimbo vya habari ni mojawapo mambo muhimu katika taharuki za kujenga mieleweko ya mwanadamu wa karne ya ishirini na moja, utamaduni na mawazo yake.
Pia matoleo mbalimbali ya kundi hilo yaliotolewa hivi mwishoni yalilengea kuwahimiza wapiganaji wa Al-Shabab baada ya kuongeza vikosi vya AMISOM na kutumia mipango mipya kwa kutaraji kuliangamiza kundi hilo na kuziokoa nchi za Afrika Mashariki kutoka ugaidi wake, pamoja na kujaribu kuimarisha uwepo wa kundi hilo nchini hizo.
Jambo linalodhihiri ni kwamba kundi hilo limechagua kutoa toleo hili katika wakati huo hasa ulio karibu na kuanza uchaguzi wa kuchagua rais mpya wa Kenya ili kuwashawishi waislamu wa Kenya kwa kudai kuwa watawala wao ni makafiri na kwamba wao ndio maadui wa Uislamu ili kuwaathiri waislamu wa Kenya wasichangia maendeleo ya nchi yao; ambapo kundi linataka kuleta hali ya mtikisiko katika jamii ya Kenya, na kuwajaalia Wakenya wawakafirishe watawala wao na kuwasha fitina baina  ya raia na watawala wao.
Kwa kweli makundi ya kigaidi yametia umuhimu mkubwa sana kwa taharuki ya kuwashawishi vijana kwa kuwa vijana hao ndio uti wa mgongo wa umma wo wote, wakiwa wenye mawazo bora na matamanio mazuri kwa nchi na anchi wenzake wataweza kuwa nguzo ya kuimarisha ustawi wa jamii na maendeleo yake, ama wakijipoteza katika giza ya mawazo makali na maoni potofu basi jamii na nchi zao labda zitapata mashaka makubwa.
Mwishoni, tunataka kuwauliza wapiganaji wa Al-Shaba na ye yote anaetaka kuwafuata baadhi ya maswali na kuashiria kwamba:
-Je, Umeridhia kutokuwa na fikiri wala kujiliwaza kwa mambo unayopatwa nayo?!
- Je, hukutambua kwamba anaye haki ya kutoa hukumu ya ukafirishaji ni Mwenyezi Mungu peke yake?! Na hakuna anaeweza kuainisha hatima ya mtu ni muumini au mkafiri.
- Vipi magaidi wa Al-Shabab watangaze kwamba watawala wa Kenya ni makafiri ilhali Mwenyezi Mungu Hakumpa ye yote haki ya kumkafirisha au kumhukumia yeyote kwa hukumu hii?
- Kisheria haijuzu kumkafirisha mwislamu ila akifanya jambo linalomtokeza nje ya Uislamu, na hata akifanya hivyo waislamu wengine wanapaswa kumwombea atubu kabla ya kumhukumia Ridda, hukumu yenyewe ni haki ya Mwenyezi Mungu au mtawala mwadilifu tu.
- Kwa hakika msingi wa Al-Walaa na Al-Baraa katika Uislamu sio kama wanavyodai magaidi wa zama hii, mwislamu anatakiwa atendeane vizuri na wanajamii wenzake wote sawa ni waislamu au wasio waislamu, pia mwislamu hutakiwa kutii watawala wake madamu hawatamlazimisha kufanya dhmbi au uhalifu.Ama kuhusu Al-Baraa haimaanishi kuwafanyia uadui wasio waislamu.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Idara ya Lugha za Kiafrika
Agosti 2017 

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.