Daesh: Utii (Al-Walaa) unamaanisha miamala tu, na pia unamaanisha upendo wa kibinadamu, ama uasi (Al-Baraa) humaanisha kumkafirisha mwengine na kumwua, kwa hiyo utii kwa mujibu wa maoni yao - unakuwa

  • | Monday, 21 August, 2017
Daesh: Utii (Al-Walaa) unamaanisha miamala tu, na pia unamaanisha upendo wa kibinadamu, ama uasi (Al-Baraa) humaanisha kumkafirisha mwengine na kumwua, kwa hiyo utii kwa mujibu wa maoni yao - unakuwa

Utii ni ahadi ya ibada, asili yake ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa kumtii pekee katika kila kitu, na pia kumpenda Mtume (S.A.W) kwa kumheshimu, kumfuata na kumnusuru, kisha kuwapenda waumini kupitia kuimarisha uhusiano wa undugu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuimarisha mieleweko ya kupendana, kuhurumiana na kusaidiana katika dini, na kunusuru nchi na kutonusuru mtu yeyote juu ya waislamu isipokuwa kwa haki, Mtume (S.A.W) Alisema: "umnusuru nduguyo awe hali ya kuwa amedhulumu au amedhulumiwa", wamesema Maswahaba watukufu: "Ewe Mtume wa Allah tumejua vipi tutamnusuru atakapokuwa amedhulumiwa, basi tuelezee vipi tutamnusuru atakapokuwa dhalimu?! "Akawaambia "kwa kumzuia asifanye dhuluma", {Bukhari: 2312}.
Kwa upande mwingine, Uasi ni jambo la ibada inayomaanisha kuwa mwislamu huchukia itikadi za kikafiri, na kuzikataa, na kujiweka mbali nazo, ambapo ni itikadi zinazotegemea kukanusha ukweli wa imani ulioletwa na Uislamu. Jambo lisilomaanisha kuwa Mwislamu anachukia kabisa wasio waislamu, na lazima tusisahau kuwa Mwenyezi Mungu katika Qurani tukufu amemzungumza na Nabii yake (S.A.W) akisema: )Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa Amtakaye. Na Yeye ndiye Anawajua zaidi waongokao).


Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.