Hakimiyah "Utawala" na tuhuma ya kuwakufurisha watawala

  • | Thursday, 24 August, 2017
Hakimiyah "Utawala" na tuhuma ya kuwakufurisha watawala

Daesh na makundi mengineyo ya kitakfiri  yanadai kwamba watawala wa nchi za kiislamu ni makafiri kwani wanaziunga mkono serikali kafiri za kimagharibi, na kuzisaidia kuwauwa waislamu, zaidi ya hayo wao hawahukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu, bali wanahukumu kwa kanuni zilizotungwa na za kisekyula, wakitegemea katika suala hilo kwa aya ya Qurani isimayo: )Na wasiohukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri(. Na kufuatia hayo basi damu yake na kila anayemsaidia juu ya ukafiri wake ni halali kumwagiwa na ni lazima kupiganiwa vita.

Kujibu tuhuma:
Kama kawaida makundi ya kigaidi yanatumia aya za Qurani kwa namna inayohudumu maslahi na ajenda zao potofu zilizo mbali sana na Uislamu, ama kuhusu aya tukufu walioitegemea katika kuwakufurisha watawala, basi Twawuus amesimulia kutoka kwa Ibn Abbas katika aya isimayo: )Na wasiohukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri(, kwamba hii si ukafiri wanaoikusudia, na katika kauli nyingine: "ni ukafiri usiotokeza nje ya mila", na katika kauli nyingine: "ni ukafiri tofauti na ukafiri mwengine, dhuluma tofauti na  dhuluma nyengine ,upotovu tofauti na upotovu mwengine". ama katika tafsiri ya Imamu Al-Qurtubi alisema kwamba aya isimayo )Na wasiohukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri( wanatumia dhahiri ya aya hiyo kama ni dalili ambao wanawakufurisha watu wanaofanya madhambi nao ni Al-Khawarij, lakini wao hawana hoja sahihi, kwani aya hiyo imeteremka katika mayahudi waliobadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyokuja katika hadithi tukufu, na hao ni makafiri, basi anashirikiana nao katika hukumu yake yule anayeshirikina nao katika sababu ya kuteremka kwake.
Imamu Ahmad Ibn Hanbal: "Ismail Ibn Saad alisema: nikamwulizia Ahmad Ibn Hanbal kuhusu kauli ya mwenyezi mungu : )Na wasiohukumu……..(, nikasema:ukafiri huo ni nini? Akasema ukafiri usiotekeza nje ya mila.
Hakika istilahi ya Hakimiyah ambayo makundi ya kigaidi yanaitegemea ili kuhalalisha upotovu wake mbali na  njia iliyonyooka, basi yanawauwa wasio na hatia na kuharibu tamaduni yakidai kwamba hakuna hukumu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu na kwamba ni lazima kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu katika ardhi. Ama kuhusu istilahi ya Hakimiyah tunasema yafuatayo:
Utawala (Al-Hakimiyah) ni istilahi ya kisasa iliyoitumiwa kwa mara ya kwanza na "Abu Al-A'la Al-Maududi" kwa ajili ya kupata uhuru kutoka mkono wa ukoloni wa Uingereza, na wakati Pakistani ilipopata uhuru wake na kujitenga na India mwaka 1947, Al-Maududi alijitenga mbali na fikra za "Hakimiyah" utawala na alifuata kanuni na katiba ya nchi bali alijiteua katika uchaguzi.
Baadaye Sayyed Qutb aliitumia fikra ile ile akitumia istilahi yenyewe baada ya kuipachika kwa mawazo yake ya kiuharibifu ili aseme kupitia kwake kwamba Misri ni nchi ya kiujinga inayoishi katika giza za ukafiri kwani haihukumiwi kwa sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Istilahi ya Al Hakimiyah "Utawala" ambayo inamaanisha kwamba hakuna hakimu "mtawala" isipokuwa Mwenyezi Mungu, yaani watawala wote wanaojitahidi katika kutunga  kanuni zinazofaa na hali na matukio mapya, wote ni makafiri; hii ni mawazo potovu, na dalili yetu juu ya hivyo ni kwamba mtume (S.A.W) aliwapa maswahaba wake haki ya kujitahidi katika zama yenye mazingira, taharuki, na mahusiano maalumu, na hakuwaambia kwamba haijuzu kwenu kubuni na kujitahidi katika kuyatatua matatizo kwani hakuna hakimu "mtawala" isipokuwa Mwenyezi Mungu! Basi vipi hali yetu ambapo maafa nyingi yaliibuka na Uislamu Ulieneza  katika maeneo mengi na sisi tupo katika karne ya 21 kwa kelele zake, matatizo yake, na maafa yake yasiyohesabika.

Hakika suala la Al Hakimiyah "utawala "kwa matatizo yaliyotokana nalo kama vile  mahojiano, matatizo, na migogoro kati ya madhehebu kama vile Khawarij, Shia'ah na wakufurishaji katika zama yetu hii,ambao  walilifahamu"utawala" vibaya , na halikuwekwa katika mahali pake, na limegeuka kutoka "utawala wa Allah "kwa "utawala wa makundi na madhehebu" yaliyoainisha nafsi yake kama kwamba ni mwenye hukumu kwa jina la Allah, yakazimwaga damu na kuzua fitina.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.