Tuhuma ya kubomoa mabaki ya kale wakidai kuwa ni masanamu

  • | Sunday, 27 August, 2017
Tuhuma ya kubomoa mabaki ya kale wakidai kuwa ni masanamu

Kundi la Daesh limedai kwamba inapaswa kuharibu na kubomoa masanamu na mabaki ya kale ya dola ya Ashuria yaliyopo mjini Mosel nchini Iraq, wakidai kuwa na masanamu, wakitegemea hadithi za Mtume (S.A.W) na kauli zilizonukuliwa kutoka kwa maswahaba zinazohalalisha suala hilo. Na labda mawazo yao hayo yanayotaka kuharibu staarabu za kiislamu na zisizo za kiislamu, ni mawazo makosa yaliyofuatiwa na Daesh na kabla yake kundi la Taliban.  


Kujibu tuhuma:


Hakika rai hii potovu zinazodai kwamba kuacha mabaki ya kale ni haramu kwani mabaki hayo ni miongoni mwa alama za ukafiri zinazowapelekea watu wadhani kwamba maneno hayo yana baraka, ni rai hizo si sahihi, kwani sheria haikuzuia kutukuza asiyekuwa Mwenyezi Mungu kabisa, bali iliyoharamishwa ni kumwabudu mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu kama walivyokuwa wakifanya watu katika zama za Ujahili walipokuwa wanaabudu masanamu yao potovu. Hivyo rai hizo potovu wanazozitegemea kundi la kigaidi hazina uhusiano wowote na dalili za kisheria, kwani kuhifadhi na kulinda ustaarabu wa kibinadamu ni jambo la lazima.
Hasa mabaki hayo ya kale katika nchi zilizofuguliwa na waislamu, yalikuwa yanakuwepo, na maswahaba hawakuamuru kuyabomoa, na wao (R.A) walikuwa wanaishi pamoja na Mtume (S.A.W) na wanajua halali kutoka haramu, bali miongoni mwa maswahaba hao waliokuja nchini Misri na wakakuta pyramids na sphinx na mabaki mengineyo na hawakutoa fatwa au rai ya kisheria inayodhuru mabaki hayo yanayozingatiwa kuwa thamani kuu ya kihistoria. Na Uislamu Ulipokuja umehifadhi urithi wa staarabu na mabaki ya kale nchini Misri, Iraq na staarabu mbali mbali yaliyotangulia Uislamu, na wameyalinda mabaki hayo mpaka tukayakuta katika siku yetu hii, na kwamba mwito wa uharibifu inaonyesha ujinga wa wasemaji wake.
Mabaki ya kale yanazingatiwa miongoni mwa thamani na vitu vya kihistoria ambayo yana athara katika jamii na umma, kwani yanaeleza historia ya umma huo, zamani na thamani yake, pia yana mawaidha kuhusu watu waliotangulia, na kwa hivyo kila anayetoa mwito wa kuharibu mabaki ya kale akidai kwamba Uislamu unaharamisha vitu hivyo katika nchi yake, basi madai hayo yanaashiria mawazo makali yanayochukuliwa kutoka  kutofahamu vizuri dini takatifu ya Uislamu.
Kuna aya na hadithi kadhaa zinazokataza kubomoa urithi wa watu wa zamani kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu: " Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya kina A'di? Wa Iram, wenye majumba marefu? Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? Na Thamudi waliochonga majabali huko bondeni?", na aya hiyo tukufu inasisitiza udharura wa kuwavuta macho ya watu kuelekea nguvu na mafanikio ya watu wa zamani, na hivyo hivyo hadithi ya Mtume (S.A.W) wakati ailpokataza kubomoa ngome za Al-Madinah.
 

Print
Tags:
Rate this article:
1.0

Please login or register to post comments.