Tuhuma ya kumkafirisha mwingine

  • | Tuesday, 29 August, 2017
Tuhuma ya kumkafirisha mwingine

      Tuhuma hii ni miongoni mwa tuhuma zinzokaririwa na makundi yenye misimamo mikali kama "kundi la Taliban Na kundi la Daesh", ili yahalalishe halifu na vitendo vyao vya kikatili, na ili kuwavuta wenye akili dhaifu na wenye hisia za kiwango cha juu, ili wajiunge nao, wakisisitiza kusema kwamba mwingine huyo ni makafiri sawa sawa akiwa anaishi India (wahindusi, wabudha, Jini na mkristo), au anaishi Pakistani sawa sawa akiwa (washia, wasufi na wakristo), maana kila asiyeiamini dini yao na mawazo yao ya kigaidi, basi awe katika mtazamo wao ni makafiri anayestahiki kuuwawa. 

Kuijibu tuhuma:

Sheria ya kiislamu inafanya kwa bidii ili kuwaachilia huru watu kutoka kila aina za kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na imeweka suala la imani na ukafiri baina ya mja na Mola wake… hakika Mtume (S.A.W) Ametufundisha kuwaamiliana na watu kwa matamshi ya ndimi zao, na tusitoi hukumu nyoyo za watu ili kuainisha muumini kutoka makafiri, kwani hakuna anayejua yaliyomo nyoyoni isipokuwa Mola wa ulimwengu… tunatoa hukumu mambo yaliyo wazi, na Mwenyezi Mungu Anajua yaliyofichwa, yeye pekee anayewahisabu waja wake. 
Ama yanayofanywa na makundi ya kigaidi kama kuwakafirisha kila anayehitilafiana nao, na kila asiyefuata mfumo wao wa kikatili basi yanamzingatia kuwa ametoka mbali na dini ya Mwenyezi Mungu. Watu hawa wanakwenda kinyume na mafundisho wazi ya Uislamu kuhusu jambo hilo, hakika Mtume (S.A.W) amemtahadharisha mwislamu kutoka kumkafirisha mwenzake au kuhalalisha kumwaga damu yake, mali yake na heshima yake.
Kundi la kikafiri linatoa istilahi ya kuritadi na ukafiri likikusudia waislamu wanaohitilafiana na rai zao potovu, ili kuhalalisha kuwauwa na kuharibu nyumba zao! Basi kutoka wapi watu hawa wamepata mafunzo yao?! na ilhali Mtume (S.A.W) amefafanua maana ya imani katika hadithi sahihi wakati Jibrili (A.S) alipomwuliza, Akasema "imani ni kumwamini Mwenyezi Mungu, malaika wake, vitabu vyake, mitume wake, siku ya mwisho na kadiri, kheri yake na shari yake", (imepokelewa na Al-Bukhari na Muslim), na pia umma wote wamekubaliana kwamba imani ni tendo la moyo, na haitoki kutoka imani ila kwa kukanusha akida iliyomwingiza katika dini hiyo. Mtume wa Mwenyezi Mungu Amesema: "mtu yeyote anapomwambia mwenzake ewe mkafiri, basi atakuwa mmoja wao ni mkafiri". (Al-Bukhari:5/2264).

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.