Tuhuma ya kutowatii makafiri miongoni mwa hukumu za Al-Walaa "utii" na Al-Baraa "uasi"

  • | Thursday, 7 September, 2017
Tuhuma ya kutowatii makafiri miongoni mwa hukumu za Al-Walaa "utii" na Al-Baraa "uasi"

     Hii ni tuhuma ambayo kundi la Daesh linaitegemea, ili kuendeleza maana ya utii na uasi kwa mujibu wa mtazamo wake kali na potovu kuhusu ukafirishaji, maana anayekataa kukubali mawazo yao uongo, anakuwa mkafiri na ameritadi. Basi katika mtazamo wao, kila miamala pamoja na asiye mwislamu inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa aina za kuacha baadhi ya mambo asili ya dini ya Uislamu kwa madai ya usamehevu wa Uislamu, na kwamba hii ni kukufuru kwa dini ya Mwenyezi Mungu inayoamuru kuwapigana vita makafiri. Na wao wanaona pia kwamba mwislamu anawajibika kutangaza uadui wake mbele na makafiri na kudhihirisha uchuki wake kwa kumwambia mkafiri: (hakika mimi nakuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu), na pia kutosaidiana nao, wala kuwashiriki katika Idi zao, na pia kutoanza kumtolea salamu kwa anayehitilafiana nao sawa akiwa (Mhindusi, Mkristo, mbudha, Msikhi, Mshia, Ahmadi...) wakitoa dalili hadithi inayosema: "msiwaanze wakristo na mayahudi kwa salamu", na pia kutoomba Mwenyezi Mungu kwao kwa kuwapa afya au kuwapa damu.


Kuijibu tuhuma:

Kwanza: Hakuna sura inayoitwa "itikadi ya Al-Walaa "utii" na Al-Baraa "uasi" katika elimu ya Tawheed, elimu ya maneno na elimu zilizofundisha itikadi ya imani kwa waislamu na kwa makundi".
pili: Al-Walaa "utii" na Al-Baraa "uasi" ni miongoni mwa vitendo vya kimoyo, inayotoka kutoka athari ya itikadi ya imani, yaani muumini anayeamini Mwenyezi Mungu, malaika wake, vitabu vyake, mitume wake, siku ya mwisho na kadiri, kheri yake na shari yake, imani hii inamzidisha upendo, utiifu na kuwanusuru waumini kwa haki, na imani inamzidisha moyo wake kujitenga mbali na itikadi na mawazo yanayopinga imani yake.
Tatu: Maana ya utii ni kunusuru na kuunga mkono, na maana ya uasi ni kufanya uadui na kutounga mkono, na alama ya utii na uasi inadhihiri sana wakati anayekufuru kwa itikadi na imani yako anapoamua kukudhulumu na kupigana vita nchi yako, hapa utii unawajibika kusimama pamoja na nchi yako, watu wako, na kutangaza uasi na maadui wanaotaka kuharibu amani ya nchi yako.
Nne: Itikadi ya utii na uasi katika Uislamu inahusiana na hali ya amani na vita, upendo na uadui, baina ya waislamu na wasio waislamu, Mwenyezi Mungu Anasema kuhusu masharti ya utii: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu(, {Al:mumtahanah.8}, na Anasema katika masharti ya uasi: {Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale waliokupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu(, {Al:mumtahanah.9}.
 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.