Muhtasari wa Taarifa ya Al-Azhar kuhusu maangamizi ya waislamu Warohinga nchini Myanmar

  • | Sunday, 10 September, 2017
Muhtasari wa Taarifa ya Al-Azhar kuhusu maangamizi ya waislamu Warohinga nchini Myanmar

- Waislamu Warohinga wanateseka kutoka uadui wa kikatili usiojulikana na wanadamu kabla ya hapo.
- Kutojali kwa mataifa ni sababu kuu ya ukiukaji huo wa kinyama dhidi ya waislamu nchini Myanmar.
- Azimio na mikataba ya kimataifa iliyojihusisha kulinda haki za wanadamu ikawa bila ya faida, bali ikawa ya uongo.
- Kwa hakika wanayoyakabili waislamu wa Rohinga inatukumbusha kwa mtindo wa wanyama wakali wa misitu.


- Kwa kweli mashirika na taasisi za kimataifa yalikuwa yatachukua hatua nyingine endapo wanaofanywa maangamizi haya miongoni mwa wafuasi wa dini nyingine isipokuwa Uislamu.
- Viongozi wa kidini nchini Myanmar wamepuuza juhudi za Al-Azhar kwa ajili ya kulitatua suala na kumaliza maangamizi, bali wakaungana na wenye misimamo mikali miongoni mwa majeshi ya nchi ili kuwafanyia waislamu mauaji wa kimbari.
- Mauaji ya kimbari dhidi ya waislamu ndiyo uhalifu mkubwa kwa historia ya Myanmar ambayo haitafutwa hata baada ya miaka kadhaa.
- Al-Azhar Al-Shareif haiwezi kubaki kimya kuhusu ukiukaji huo usioambatana na ubinadamu.
- Al-Azhar Al-Shareif itaongoza juhudi za kuanza taharuki ya kibinadamu kwa kiwango cha mataifa ya kiarabu na ya kiislamu na hata kiulimwengu kwa ajili ya kumaliza maangamizi hayo.
- Jinai jama hizo zinachochea kuzuka vurugu na kueneza ugaidi ambao ulimwengu wote unateseka sana kutokana na hatari na athari zake mbaya.
- Tunataka kutoa wito wa kibinadamu kuomba kumaliza sera ya ubaguzi kwa msingi wa dini baina ya wananchi.
- Tumehuzunika sana kuona aliyepata zawadi ya "Nobel" ya kueneza na kuhimiza amani mkononi mwake, anachochea kuwaua na kuwaangamiza watu wasio na hatia akipuuza haki ya watu hao kuishi kwa amani na utulivu.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.