kuhalalisha Daesh kuhusu kuwaua watu wanaohitilafiana nao kwa kuwachoma moto

  • | Sunday, 10 September, 2017
kuhalalisha Daesh kuhusu kuwaua watu wanaohitilafiana nao kwa kuwachoma moto

     Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewatukuza wanadamu wakiwa hai au wamekufa, kwa hivyo Mwenyezi Mungu Anasema: {Na hakika tumewatukuza wanadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tuliowaumba}, na miongoni mwa mifano ya kutukuza Mwenyezi Mungu kwa wanadamu, ni kwamba Amefanya kumwokoa mtu asiye na hatia kutoka mauti ni kama kuwahuisha watu wote, na kumwua mtu kama kuwaua watu wote, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu:{Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliyemuuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote}, yaani anayelinda uhai wa mtu mmoja kupitia msamaha wake au anazuia kumwua au kumwokoa kutoka baadhi ya sababu za maangamizi, basi anakuwa kama amewaokoa watu wote, na makusudio ya hayo: ni kuharamisha kuua nafsi ya kibinadamu na kuogopesha kumfanyia mtu madhara na kuhimiza kumlinda mwanadamu.
Hakika Uislamu Umekataza kuharibu miili ya waliokufa, au kumchoma moto mtu akiwa hai au amekufa, kwani katika kitabu cha Musnad Imamu Ahmed ametaja hadithi ya Mtume (S.A.W) inayosema: "kwamba Mtume wetu (S.A.W) alikuwa anakataza kuharibu miili ya waliokufa", na katika kitabu cha Al-Bukhari, Abu Hurayrah amesema: Mtume (S.A.W) Ametutuma katika safari na Akituambia: "mkikuta Fulani na Fulani –anakusudia watu wawili kutoka Quraish na ametaja majina yao- basi muwachome kwa moto" Abu Hurayrah akasema: kisha tukamjia Mtume (S.A.W) ili kumaga tulipotaka kutoka, na Akasema: "Mimi nilikuwa nikawaamuru kuwachoma moto mtu fulani na fulani, na kwamba Mwenyezi Mungu pekee yake Ana haki ya kuadhibu kwa moto, basi mkiwakuta watu hawa muwaue".
Bali hakika Uislamu unakataza kuwachoma moto wadudu, hivyo vipi Uislamu Unakubali kuwachoma moto watu waliotukuzwa na Mwenyezi Mungu?!!, imepokelewa kutoka kwa Ibn Masuud (R.A) kwamba amesema: "tulikuwa pamoja na Mtume (S.W.A) kisha tukafika kwenye chuguu za wachwa zilizochomwa moto, basi Mtume akasema: "haijuzu kwa mtu yeyote kuadhibu kwa kutumia moto isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu". 
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.