Kundi la Daesh linamtukuka kiongozi wake na linamsifu kama ni amiri wa waumini na khalifa wa Mtume (S.A.W), hivyo wafuasi wa Daesh wanazitii amri zake na wanaacha mambo aliyoyakataza

  • | Thursday, 14 September, 2017
Kundi la Daesh linamtukuka kiongozi wake na linamsifu kama ni amiri wa waumini na khalifa wa Mtume (S.A.W), hivyo wafuasi wa Daesh wanazitii amri zake na wanaacha mambo aliyoyakataza

     Mwandishi ametaja katika makala ya "njia za kushinda", sehemu ya pili, toleo la tano kutoka gazeti la Rumia, kwamba miongoni mwa sababu za kushinda ni kumfuata amiri wa waumini na kumtii katika hali zote. Akitoa dalili kwa hadithi ya Ubadah Ibn Al-Samet (R.A) ambapo alisema: ''tumempa bai‘ah Mtume (S.W.A) juu ya kusikia na kutii wakati wa shida, wepesi na katika hali ya kupenda, kufanya wema na katika hali ya kizembe, na pia tumempa bai‘ah Mtume (S.W.A) juu utii hata likiwa jambo hilo halipendezwa na nafsi, na pia hatushindani mtawala isipokuwa tukiona ukafiri wazi wazi, pia tutasema haki bila ya hofu''. Kisha mwandishi anatoa dalili juu ya kutojuzu kujitahidi hata ikiwa jitihadi ni sawa, ili matokeo ya jitihadi hiyo yasipingane na amri za amiri.
Na ametaja kwamba miongoni mwa njia za kuhakikisha kumtii amiri:
1-    kumdhania njema amiri.
2-    kumheshimu amiri na kumtukuka na kutaja mazuri yake.  
Hiyo inamaanisha kwamba jambo limetoka mbali na hali ya utii, na limefika kwenye hali ya utumwa, basi hakuna jitihadi pamoja na amri za amiri wa waumini, wala hawashindani naye kuhusu mambo ya utawala, wala hawamtaja isipokuwa kwa wema na amiri huyo kutoka mtazamo wao yuko juu ya okosoaji, maana anjisifu yeye na amri zake kwa sifa za utukufu.
Na jambo hilo halihusiani na Uislamu kamwe, pia Mtume (S.A.W), maswahaba wake na makhalifa walioongoka hawakufanya mambo hayo, na tunataja kuhusu suala hilo mifano kadhaa ambapo maswahaba walikuwa wanampinga Mtume (S.A.W) katika suala yasiyo ya kisheria na yasiyokuja kupitia Wahyi:
1- imepokelewa kutoka kwa Abi Said Al-Khudri (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) Amesema: "tahadharisheni msiketi njiani". Maswahaba wakasema: "ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hatuna budi kuketi katika mabaraza yetu tunazungunza. Mtume (S.A.W) Akawaambia "iwapo hamna njia isipokuwa kuketi, basi ipeni njia haki yake", wakauliza: "ni ipi haki ya njia Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Akajibu "ni kuinamisha macho (kutotazama yaliyoharamishwa), kuondoa udhia, kurudisha salamu, kuamrisha mema na kukataza mabaya". Imekubaliwa na wote.
2- imepokelewa kutoka kwa Al-Habbab Ibin Al-Munzir Ibin Al-Gamuuh amemwambia Mtume (S.A.W) wakati wa vita ya Badr kuhusu kuchagua mahali pa vita: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je Mwenyezi Mungu Amekuamuru kuchagua mahali hapo, basi tutafuata amri hii moja kwa moja, au sababu ya kuchagua mahali hapo ni ushauri, vita na udanganifu?, Mtume (S.A.W) Akasema: "bali ni ushauri, vita na udanganifu", akasema: "ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mahali hapo si nzuri, basi twende mpaka tufike kwenye kisima cha maji ambacho watakaokifika kwanza, na tuanzishe kambi yetu, kisha tutaziba visima vyote, baadaye tutajenge tuta karibu na kisima hicho na tutaijaza kwa maji, basi wakati huo tutawapigana vita watu, na tutaweza kunywa na wao hawatakunywa", Mtume (S.A.W) Akasema "umetoa rai nzuri", Mtume (S.A.W) Aksimama yeye na watu walio pamoja naye na wakaenda hadi wakafika karibu na kisima kilicho karibu sana na maadui, kisha Akajenga tuta karibu na kisima hicho na Akaweka maji katika tuta hilo baadaye Akaziba visima vyote.
3- Na pia siku maalumu Umar Bin Al-Khattab alitoa hotuba akasema: "msiainishe mahari kubwa kwani mahari ingalikuwa tendo la kheri duniani au tendo la kumcha Mungu, basi Mtume angaliifanya, ambapo Mtume hakuainisha mahari kwa wanawake wake wala mabinti wake zaidi ya wakia "mizani "kumi na mbili. Basi wakati wa hotuba wa Umar Bin Al-Khattab mwanamke mmoja akasimama na kusema: "ewe Umar, Mwenyezi Mungu Anatupa na wewe unatuzuia, je! Mwenyezi Mungu Amesema: {Na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote}, Umar Akasema: mwanamke amesema kweli na Umar amekosea.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.