Al-Azhar Al-Shareif yatoa wito kwa kuwaokoa waislamu wa Rohinga kutoka uadui na maangamizi

  • | Friday, 15 September, 2017
Al-Azhar Al-Shareif yatoa wito kwa kuwaokoa waislamu wa Rohinga kutoka uadui na maangamizi

     Japokuwa hali ya kukaa kimya iliyotawala ulimwenguni kote kuhusu maangamizi yanayowapata waislamu walio chache wa Rohinga kwenye jimbo la Rakhin, nchini Myanmar Al-Azhar Al-Shareif hakusita kutoa wito kwa kuwasaidia wanyonge hawa, ambapo taasisi hiyo iliyo kubwa zaidi katika uilimwengu wa kiislamu ilianza taharuki kubwa kwa ajili ya kulitatua tatizo hilo gumu. Kwa kweli taharuki na juhudi za Al-Azhar Al-Shareif hazianza ghafla wala mchelewa, bali tangu mwanzo wa kuzuka mzozo na kuanza ukiukaji dhaidi ya waislamu wa Rohinga, ambapo ilitoa taarifa na wito kadhaa ili kutafuta suluhisho mwafaka kwa janga hilo la kibinadamu.

Image

 


Al-Azhar Al-Shareif ilieleza kukataa kwake na kupinga kwake kwa vitendo vya kiadui na maangamizi inayoyafanya serikali ya Myanmar pamoja na baadhi ya Mabudhi wanao misimamo mikali dhidi ya waislamu wa Rohinga, ikitoa wito mbali mbali kwa jumuiya za kupitisha hatima duniani kama vile; Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama, nchi kuu, mashirika ya kutoa misaada na yanayohusiana na kazi za kuokoa wananchi ili wapate msaada wa dharura na kutekeleza majukumu yao kulingana na wanyonge hao.

Image

 


Isitoshe, Al-Azhar Al-Shareif imetoa wito kwa wahusika wa serikali wa Myanmar na wajumbe wa waislamu wa Rohinga waje hapa Misri ili wajadiliane kwa ulezi wa Al-Azhar Al-Shareif na Baraza la Wakuu wa waislamu kwa lengo la kuerdisha maelewano baina ya pande mbili na kutafutia suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo.
Ifikapo mwezi wa January mwaka huu mkutano wa kujadili suala la mateso ya waislamu wa Rohinga umefanyika mjini Kairo kwa ulezi wa pamoja baina ya Al-Azhar Al-Shareif na Baraza la Wakuu wa waislamu, ambapo mkutano huu ulikuwa ndio tukio la kwanza kabisa linalowajumuisha wajumbe wa pande za mgogoro huko Myanmar, wakajadiliana kuhusu sababu za mzozo na njia za kufikia suluhisho.
Kwa kumalizika kwa mkutano huo Al-Azhar Al-Shareif na ulimwengu wote wakawa na tamaa ya kuwa serikali ya Myanmar italazimika kwa makubaliano na maamuzi ya mkutano huo, lakini kwa bahati mbaya seriakali haikufanya hivyo, bali imepuuza kila linalotokana na mkutano na mijadala, kwa upande wake, Aung San Suu Kyi kiongozi wa Myanmar ameendelea katika kuchochea wapiganaji wake na wanao misimamo mikali miongoni mwa mabudha kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya waislamu wa Rohinga na kutekeleza mikakati ya kikatili dhidi yao, na hakuchukua hatua yo yote inayoweza kuchangia kusimamisha zile jinai na maangamizi, zaidi ya hayo alipoalikwa kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Matiafa (UN) mwezi huu hakuhudhuria jambo linalozidisha lawama zinaomkabili.
Al-Azhar haikukata tamaa ikatoa taarifa ya kihistoria ikitoa wito kwa ulimwengu kote uchangia kulitatua suala hilo ambapo Imamu Mkuu Profesa; Ahmad Al-Tayyib alitoa taarifa ya kutaka msaada wa jamii ya kimataifa kutekeleza majukumu yake kuhusu suala hilo.
Kwa hakika suala la kuwafanyia waislamu wa Rohinga ukatili na mateso halina budi kujadiliwa kwa viwango vyote mpaka ulimwengu kote utambue ukweli wa suala hilo na jamii ya kimataifa itekeleza wajibu zake kwa wanyonge hao. Ama Al-Azhar Al-Shareif itaendelea kutetea haki ya wanyonge hawa na wanyonge wote duniani kuishi kwa amani na kusikia raha na utulivu nchini mwao.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
1.0

Please login or register to post comments.