Suala la kuvaa (Shela) Niqaab

  • | Sunday, 17 September, 2017
Suala la kuvaa (Shela) Niqaab

     Katika wakati huu tuhuma zinazohusiana na (Shela) Niqaab zinajadiliwa sana na kusema kwamba ni uzushi ulioingizwa katika jamii ya kiislamu, ilhali ukweli ni kwamba tuhuma hii ni kinyume cha kauli isemayo kwamba kuvaa Niqaab ni faradhi juu ya kila mwanamke, na ikiwa kauli isemayo kwamba kuvaa niqaab ni faradhi ni ya baadhi ya wanavyuoni, basi kauli isemayo kwamba niqaab si wajibu na kwamba inajuzu kwa mwanamke kudhihirisha uso na mikono miwili yake mbele ya wanaume wageni ni rai ya kundi la wanavyuoni waitwao "Al-Jumhuur".
Na akiwa aliyesema kwamba kuvaa niqaab ni wajibu ana dalili anazozitegemea, basi dalili hizo ni za kiwango cha chini zikilinganishwa na dalili za Al-Jumhuur.
Miongoni mwa dalili wanazozitegemea Al-Jumhuur kwamba kuvaa niqaab si wajibu ni kauli ya Mwenyezi Mungu katika sura ya Al-Nuur: )wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika(, {Al-Nuur:31}. Na Al-Jumhuur walisema kwamba maana ya )isipokuwa unaodhihirika(, ni uso na mikono miwili, wanja na pete na mahali panapofanana na hapo kati ya mahali pa kudhihirisha mapambo. Na hii imepokewa kutoka kwa Anas Ibn Malik, na Ibn Abbas, na Bibi Aisha, na Ikrimah, Saidi Bin Jubair, Ataa na Qatadah na Al-Musawir Ibn Makhrumah (R.A.).
Vile vile, Al-Jumhuur walitoa dalili kwa kauli ya Mwenyezi Mungu kuhusu hali ya waumini wanawake: )Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao(, {Al-Nuur:31}. Na shungi ni: kifuniko cha kichwa, kwa hivyo Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha wanawake waangushe na waweke vifuniko kwa namna inayofunika shingo na vifua kikamili. Na ikiwa kufunika uso ni wajibu, kungalitajwa wazi wazi katika aya na kuamuru kuangusha shungi zao juu ya nyuso zao, kama ilivyoeleza kwa kuangusha juu ya vifua.
Ama wanaosema kuwa niqaab ni wajibu basi walitoa dalili kwa iliyopokewa kutoka kwa Ibn Mas’uud kuhusu tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: )wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika(, {Al-Nuur:31}, kwamba maana yake ni nguo na mavazi yaliyo dhahiri.
Lakini Al-jumhuur walijibu kwamba tafsiri hii inapingana na rai zilizo sahihi zilizopokelewa kutoka kwa maswahaba (R.A.).
Isitoshe, bali walitoa dalili kwa iliyopokewa kutoka kwa Imamu Ahmad na Al-Bukhari kutoka kwa Ibn Umar kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: "mwanamke anayehiji havai niqaab, na wala havai glovu" na dalili hiyo inathibitisha kuwa mwanamke wasiyekwenda Hajj hupaswa kuvaa glovu mbili.
Lakini Al-Jumhuur walijibu kuhusu hadithi hii kwamba uso na mikono miwili sio uchi, kwani vipi inajuzu kudhihirishwa uso na mikono miwili, ilhali ibada haiwi sahihi wakati wa kudhihirisha uchi. Na kwani kudhihirisha uchi ni sababu mojawapo sababu za kubatilisha Ihraam pamoja na kuvaa nguo za kawaida na kuwinda na mengine, na mambo hayo mawili sio wajibu kisha yamekuwa haramu yakifanywa wakati wa Ihraam lakini hayo ni miongoni mwa mambo halali.
Na maoni ya Al-Jumhuur kwamba kuvaa niqaab kwa mwanamke sio sababu yake kufunika mahali pa aibu pasionekana hayamaanishi kuwa inajuzu kumwadhibu mwanamke asiyeivaa mpaka avue, lakini msingi ni kwamba "Kuvaa Niqaab ni jambo ambalo halina maagizo wala makatazo ya wazi wazi".

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.