Daesh: waislamu wanapaswa kutokubali mfumo wowote wa kisiasa isipokuwa Khilafa iliyoletwa na Uislamu

  • | Tuesday, 19 September, 2017
Daesh: waislamu wanapaswa kutokubali mfumo wowote wa kisiasa isipokuwa Khilafa iliyoletwa na Uislamu

      Mfumo wa utawala katika Uislamu hutegemea hali ya watu na desturi zao kwa sharti ya kutokuwa na kanuni  inayopinga sheria ya Mwenyezi Mungu (S.W), ambapo haikuwepo aya moja au hadithi moja wazi na sahihi inayowalizimisha waislamu kusimamisha mfumo maalumu wa kisiasa, bali zilikuwepo aya na hadithi zilizotaja ulazima wa kutekeleza uadilifu na kuzichunga maslahi za waja na nchi kwa namna inayomridhia Mola wa watu.
    Mifumo yote ya kiutawala iliyokuja baada ya zama za makhalifa waongofu Abu Bakr, Omar, Othman, Ali na Al-Hassan Bin Ali haiitwi Khilafa isipokuwa katika mtazamo wa kilugha tu, ama kwa upande wa ukweli wake basi mifumo hiyo ndiyo ilikuwa mifumo mbali mbali ya utawala, jambo linalothibitisha kwamba mifumo ya utawala inatofautiana katika Uislamu kwa mujibu wa tamaduni, mila na desturi na hali.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.