Daesh: kuwasiliana na kutendeana na asiye mwislamu inavunja msingi wa utii "Al-Walaa" na uasi "Al-Baraa" katika Uislamu

  • | Monday, 25 September, 2017
Daesh: kuwasiliana na kutendeana na asiye mwislamu inavunja msingi wa utii "Al-Walaa" na uasi "Al-Baraa" katika Uislamu

      Kutendeana na asiye mwislamu na kusaidiana naye katika mambo, maslahi za pamoja haiwezekani kuwa haramu, na dalili ya hayo ni kwamba Mtume (S.A.W) alitendeana na akawasiliana na wasio waislamu na hakukataza kufanya hivyo, bali Qurani Tukufu imesema: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu… Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu}.
Basi dini yetu haituamuru kufanya uadui dhidi ya wasio waislamu na kutendeana nao kwa nguvu na vurugu isipokuwa katika hali ya kujitetea na kujibu mashambulizi yao, na hilo ni jambo linalokubaliwa na akili nzima, ama wakiwa waislamu katika hali ya kupitisha amani na wasio waislamu, basi wanapaswa kutekeleza hukumu za aya takatifu kama kuwafanyia wema na uadilifu.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.