Daesh: Khilafa ni wajibu wa kisheria isiyokubali kuwepo mfumo mwingine wa kisiasa na kwamba Khilafa ndio mfumo wa pekee wa utawala katika Uislamu

  • | Sunday, 1 October, 2017
Daesh: Khilafa ni wajibu wa kisheria isiyokubali kuwepo mfumo mwingine wa kisiasa na kwamba Khilafa ndio mfumo wa pekee wa utawala katika Uislamu

     Khilafa katika lugha ni kutoka tamko la خلفه يخلفه kwa maana ya alimfanya nyuma yake basi yeye ni خليفة naye ni yule anayefuata aliyemtangulia.
Na katika Istilahi khilafa ni: kuendesha mambo ya dunia na kuwachunga waja kwa mujibu wa sharia za Mwenyezi Mungu (S.W).
Jukumu la kwanza lililo muhimu la khilafa ni kuendesha mambo ya dunia kwa mujibu wa mafunzo ya dini na kuhifadhi dini na kuichunga, hivyo yeyote akidai kuwa alijitangaza khilafa pasipo na kujilazimika na majukumu yake, basi yeye ndiye mwongo dhahiri.
Khilafa katika Uislamu ni mfumo wa kisiasa usiokusuduwi kwa maana dhahiri yake, bali hukusudiwa kwa madhumuni yake hata ukiitwa kwa jina jingine mbali na neno la Khalifa.
Tamko la Khalifa katika lugha huhusiana na kila mtawala anayekuja baada ya mtawala mwingine, na katika istilahi tamko hilo huhusiana na yule aliyemfuata Mtume (S.A.W.) katika kuendesha mambo dunia kwa mujibu wa dini "makhalifa waongofu".
Imamu Attirmidhiy alisimulia katika kitabu chake [Al-Sunan] na imamu Annasaaiy, Abu Dawood na Ahmad katika kitabu chake cha Musnad kwa matamshi yanayofanana ya kauli yake Mtume (S.A.W.): "khilafa utakuwepo katika umma wangu kwa miaka thelathini, kisha itakuwa mfumo wa ufalme baada ya hapo" maana khilafa utakuwepo katika zama za utawala wa makhalifa waongofu Abu Bakr, Omar Bin Al-Khattab, Othman, Ali Bin Abi Talib na Al-Hassan Bin Ali (R.A.), ambapo mifumo yote ya kisiasa iliyokuja baada yao katika maana ya istilahi ndiyo ufalme na utawala na sio khilafa wa kidini kutoka kwa Mtume (S.A.W.) bali watawala  walipewa jina la khalifa kwa kuzingatia maana ya kilugha ambapo walifuata watawala waliowatangulia.  

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.