Kwa hakika walichukua vipande vya baadhi ya matini za kisheria wakipuuza kwa makusudi vipande vingine kama vile zile hadithi zinazokanusha uwajibu wa kuhama "Hijrah", kama kauli yake Mtume (S.A.W) iliyosimuliwa na Al-Bukhari kutoka kwa Ibn Abbas (R.A) kwamba Mtume Akasema: "hakuna Hijrah baada ya kuingia Makkah, lakini kuna Jihadi na nia, mtakapotakiwa kwenda kupiga jihadi basi nendeni". Na kauli yake Mtume (S.A.W) kwa mtu aliyemjia kuomba ruhusa yake ili ahame "Hijrah" iliyosimuliwa na Al-Bukhari: "hakuna kuhama "Hijrah" baada ya kuingia Makkah, lakini nitampa ahadi juu ya Uislamu"1 , na kwamba wanachuoni wamekusanya baina ya hadithi hizo kwa kusema: hakika kuhama "Hijrah" ilikwisha baada ya kuingia Makkah.
____________________________
1 Sahihul Bukhari 2913