Daesh: Kutowakufurisha wafanyao madhambi hasa watawala wasiohukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa vitendo vya kundi la Murji’a na sio miongoni mwa vitendo vya Ahlul-Sunna na Jamaa

  • | Sunday, 8 October, 2017
Daesh: Kutowakufurisha wafanyao madhambi hasa watawala wasiohukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa vitendo vya kundi la Murji’a na sio miongoni mwa vitendo vya Ahlul-Sunna na Jamaa

     Madhehebu ya Maimamu wa waislamu kutoka enzi ya Mtume Muhammad (S.A.W) mpaka siku ya hivi sasa yanaeleza kwamba anayefanya madhambi hata yakiwa ni madhambi makubwa hubaki Mwislamu na ni lazima tuombe dua Mwenyezi Mungu ampe toba na uongofu. Msingi huo ulikubaliwa na wote isipokuwa kundi la Al-Khawarij ambao waliwakufurisha waislamu wanaofanya madhambi, bali hata waliwakufurisha Maswahaba wa Mtume (S.A.W) kwa sababu ya madhambi waliyoyafanya, kwa hivyo si jambo la ajabu kwamba wafuasi wa kundi hilo walikufurisha jamii ya kiislamu ulimwenguni kote katika siku za hivi sasa, hakika historia ya mawazo ya kuwakufurisha wanaofanya madhambi yanarejea moaka enzi ya kundi la Al-Khawarij waliomwasi Bwana wetu Imamu Ali ibin Abi Twaleb na wakamkufurisha yeye na maswahaba wengi kwa madai ya kwamba wamefanya madhambi na hatia.
Na sisi hatusahau kauli za Mtume (S.A.W.) alipoonya sana kutoka Ukufurishaji kwa ujumla ambapo alisema katika hadithi yake sahihi: "Mtu yeyote anayemwita nduguye kuwa ni mkafiri basi mmoja miongoni mwao huwa ni mkafiri", na hiyo ni onyo kali kutoka ukafirishaji na hatima yake.
Hakika wito hiyo ni dalili kwamba makundi yenye mawazo makali yanachagua mifano mibaya au mifano isiyo sawa kupitia historia ya kiislamu kisha wanaizalisha mifano hiyo upya, basi wanakosa na hupatwa na hasara kama walivyofanywa waliotangulia.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.