Taarifa ya Al-Azhar kuhusu madai ya kuwaua wanajeshi na polisi

  • | Monday, 23 October, 2017
Taarifa ya Al-Azhar kuhusu madai ya kuwaua wanajeshi na polisi

Kudai kwamba: kuwauwa wanajeshi na Polisi ni Jihadi
Jibu:

Jihadi iko mbali -sana- na wanayoyadai wahalifu na waharibifu hao, basi Jihadi ina maana nzuri sana, lakini wafisadi hao hawaijua maana yake, kwani maana yake ni kutoa juhudi kupambana nasfi katika mambo yanyoidhuru au kudhuru wengine, au katika mambo mengine katika maisha yetu. Pia kupambana na Shetani ambaye ni adui dhahiri kwa mwanadamu - ni Jihadi ya juu- au kutoa juhudi kujibia mashambulizi, na aya inayosisitiza hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu: ﴾Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui﴿, [Al-Baqarah:190]

 

Image

 

Basi Jihadi ni njia ya kujibia mashambulizi, na haifai kuwa Jihadi ni njia ya uadui.
Ama yanayofanywa dhidi ya wanajeshi na polisi yanazingatiwa ugaidi wala hayahusiani na Jihadi kamwe, bali unachafua maana ya Jihadi nzuri.
Hakika Jihadi ya kweli ni ile inayotekelezwa na wanajeshi na polisi kwa ajili ya kuishia wahalifu na waharibifu, na kulinda nyumba, nafsi, mali na nchi.
Basi usidanganyike ndugu wangu kijana kwa madai yanayosema kwamba kuwauwa wanajeshi na Polisi ni Jihadi, ukweli siyo Jihadi bali ni uharibifu na ugaidi.
Na hii inawalazimisha watu wote katika jamii kujitahadhari kwa ajili ya kushinda ugaidi huo na kujiokoa kutoka shari zake.
Mwishoni tumwombie Mwenyezi Mungu ailinde nchi na waja kutoka kila baya na awalinde wanaoishi katika amani kutoka wanaopanga  vibaya na makhaini.

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Kitengo cha Lugha za kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.