Mke wa Rais wa Chad: Al-Azhar ina cheo cha juu sana nyoyoni mwa wananchi wa Chad na Waafrika wote

  • | Monday, 23 October, 2017
Mke wa Rais wa Chad: Al-Azhar ina cheo cha juu sana nyoyoni mwa wananchi wa Chad na Waafrika wote

     Mhwshimiwa Imamu Mkuu wa Al-Azhar Al-Shaerif Profesa/ Ahmad Al-Tayyib amempokea leo Bibi/ Henda Diby Etno mke wa Rais wa Chad aliyeanza ziara nchini Misri. Katika mkutano huo Imamu Mkuu alimkaribisha Bi.; Etno kwenye Al-Azhar Al-Shareif akisisitiza kwamba mahusiano yaliyopo baina ya Al-Azhar na Chad ni mahusiano imara na yenye historia ndefu, kupitia mamia ya wanafunzi wa Chad wanaosoma katika vitivo mbali mbali vya Chuo Kikuu cha Al-Azhar na Taasisi zake, pamoja na walimu wa Al-Azhar wanaotumwa nchini Chad ili kuwasomesha wanafunzi wa huko, licha ya misafara ya matibabu inayopelekwa na Al-Azhar kwa ajili ya kuwasaidia wachad kupata matibabu kutoka maradhi na wanaohitaji misaada, zaidi ya hayo Al-Azhar inapeleka misafara ya kilinganiaji kwa kuwasaidia waislamu wa Chad kufahamu masuala ya dini yao na kuwa na maarifa makubwa kuhusu dini na sheria za kiislamu.
     Mheshimiwa Imamu Mkuu aliamua kuongeza tuzo za kupata mafunzo kwa wanafunzi wa Chad na kuzigawanya tuzo hizo baina ya vitivo mbali mbali vya Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambapo sehemu ya tuzo hizo itahusishwa kwa wanafunzi wa wanaotaka kusoma elimu za sayansi kama vile; Utibabu, Utengenezaji dawa, Uhandisi n.k., ama sehemu ya pili itahusishwa kwa wale wanaotaka kusoma elimu za kisheria na kiarabu kama vile; Usuul El-Diin, Lugha ya Kiarabu n.k.
     Vile vile, Imamu Mkuu alimwambia Bi.; Etno kuwa Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kuwapokea maimamu wa Chad na kuwapa matayarisho na mazoezi yenye hali ya juu ili waweze kutoa hotuba inayosaidia kupambana na fikira za kigaidi na kuamiliana na masuala na changamoto za kisasa.
     Kwa upande wake, Bi.; Henda Diby Etno mke wa Rais wa Chad alitoa shukrani zake na heshima yake mkubwa kwa misaada inayotolewa na Al-Azhar Al-Shareif kwa nchi yake hasa katika uwanja wa elimu na mafundisho, mazoezi, kazi ya kutoa huduma za wanadamu inayofanywa na Al-Azhar nchini Chad, akisifu sana juhudi za Al-Azhar kueneza amani na usalama duniani na kupambana na mawazo makali, akisisitiza kuwa Al-Azhar Al-Shareif ina cheo cha juu sana nyoyoni mwa wananchi wa Chad, na pia waafrika na malimwengu kote.
 
 
Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Kitengo cha Lugha za kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.