Balozi wa Tanzania nchini Misri amaliza kipindi cha kazi yake kwa kukutana na Imamu Mkuu

  • | Monday, 23 October, 2017
Balozi wa Tanzania nchini Misri amaliza kipindi cha kazi yake kwa kukutana na Imamu Mkuu

     Mheshimiwa Imamu Mkuu Profesa, Ahmad Al-Tayyib Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif alimpokea leo Bwana, Muhammed Al-Haj Hamza Balozi wa Tanzania mjini Kairo kwa mnasaba wa kumalizika kwa muda wake wa kidplomasia hapa Misri. Imamu Mkuu alimkaribisha Bwana Hamza kwenye Al-Azhar Al-Shareif akimtamani mafaniko zaidi katika muda zijazo za kazi yake ya kidplomasia.
     Imamu Mkuua alisisitiza katika mkutano huo kwamba Al-Azhar ina uwezo wa kuzidisha misaada kwa waislamu wa Tanzania kupitia kuongeza idadi ya tuzo za kusoma katika Al-Azhar zinazohusishwa kwa wanafunzi wa Tanzania kwa ajili ya kujifunza katika vitivo vya kisheria na vya kisayansi, na pia kupitia kuwasaidia maimamu wa Tanzania kupata mazoezi na maarifa mapya yanayoweza kuwawezesha kupambana na masuala ya kisasa na hasa fikira za kigaidi na matatizo magumu yaliyoenea ulimwenguni kote na hasa barani Afrika kama vile; vurugu, migogoro, misimamo mikali n.k.

      Kwa upande wake, Bwana, Muhammed Al-Haj Hamza alisema kuwa mbinu wa Al-Azhar Al-Shareif unaotegemea kukubali maoni mbali mbali na kuziheshimu rai tofauti ulihifadhi utulivu wa jamii sio nchini Misri tu, bali katika ulimwengu mzima, na hasa barani Afrika, ambapo Al-Azhar Al-Shareif ilikuwa na roli muhimu sana katika kueneza dini kwa njia iliyo bora zaidi na kuwapa waislamu duniani ufahamu sahihi na mawazo yaliyo sawa kuhusu dini hiyo takatifu kupitia wajumbe wa Al-Azhar waliowahi kusambazwa barani Afrika, na kuwapokea wanafunzi kwa ajili ya kusoma na kujifunza katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar. Pia, Bwana Hamza aliashiria kuwa nchi yake inataraji kuzidisha na kuimarisha nyanja za ushirikiano pamoja na Al-Azhar Al-Shareif katika nyanja mbali mbali, kwani inatambua na kuzingatia sana umuhimu wa Taasisi hiyo na athari zake zilizo wazi katika wahitimu wake wanaotekeleza jukumu muhimu kabisa katika jamii ya Tanzania kwa kueneza amani ya kijamii na kuisaidia nchi yao ipate utulivu na maendeleo.  

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Kitengo cha Lugha za kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.