Udugu wa Mitume Uislamu wa kimataifa (3)

  • | Tuesday, 24 October, 2017
Udugu wa Mitume Uislamu wa kimataifa (3)

     Mwenyezi Mungu (S.W) Ametaka ujumbe wa Mtume Muhammad (S.A.W) uwe mwisho wa jumbe za mbinguni, na ujumbe huo uliotremshwa na Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wetu Mohammad (S.A.W) umefika daraja juu ya kukamilika, na ulikuja kama ulinganio wa kibinadamu na kiulimwengu, hauwazungumzi watu wala taifa maalumu, na baada ya ujio wa Mitume na Manabii wanaobeba bendera ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kila mmoja anawaambia watu wake: {Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni Mwonyaji niliyedhahiri kwenu}[Nuuh:2], na kauli yake (S.W): {akasema: "Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye}[Al-A’araaf:59]….nk, basi ametumwa mwisho wa Mitume na Amekusanya jumbe zote chini ya bendera moja, na ameendelea kuwaita watu wote akisema {Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu; ili mpate kuokoka}[Al-Baqarah:21], na kauli yake M.M {Enyi watu! lmekuflkieni dalili kutoka kwa Mola wenu}[Al-Nisaa’:174] na kauli yake M.M {Haya yatosha (kuwa mauidha) kwa watu, ili waonywe kwayo}[Ibrahiim:52], yaani ni mawaidha kwa kila aliyepata habari ya ujumbe wa Mtume mpaka siku ya Qiyama: {Na Qurani hii imefunuliwa kwangu ili kwa hiyo nikuonyeni nyinyi na kila imefikiayo} [Al-An’aam:19] na Jini na wanadamu ni sawa katika aya hii: {Enyi jamii ya majini na watu}, [Al-rahman: 6].
      Pia kuna aya kadhaa zinazotangaza kwamba Qurani ni ukumbusho kwa walimwengu wote, kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu: {Hayakuwa haya (uliyokuja nayo) ila ni mauidha kwa walimwengu wote}[Yusuf:104], na kauli yake {Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu} [Al-Qalam:52].
     Hakika ujumbe wa Uislamu ulioletwa na Mtume Muhammad (S.A.W) umezindua dhana ya ulimwengu inayomaanisha kwamba dini ni moja kutoka mwanzo wa dunia mpaka siku ya Qiyama, na kwamba Mitume ni wadugu katika kazi ya kuwaongoza watu kwenye njia ya Mwenyezi Mungu na kuwapa dalili juu ya kuwepo kwake… na kwamba Qurani Tukufu imekusanya kila kilichosemwa na Mitume kama vile itikadi na fadhila, kwa hivyo ni lazima kuwaamini Mitume na Manabii wote, na kumkufuru mmoja wao ni kama kukanusha ujumbe wa Mtume Mohammad (S.A.W) mwenyewe, na lengo la hayo yote ni kuwazuia waislamu kumdharau mmoja miongoni mwa Mitume, au kutokea uadui baina yao kwa sababu ya Mitume, na kwa hivyo Mtume Mohammad (S.A.W) Amekataza sana kuwepo upendeleao kwa sababu ya ukabila, rangi, nguvu, au utajiri, na kiina cha Uislamu ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu "Tawhiid", ibada, sheria na utii "Al-Walaa", Mwenyezi Mungu Amesema: {Na yametimia maneno ya Mola wako kwa kweli na uadilifu. Hakuna awezaye kuyabadilisha maneno Yake}.
     Hakika maadili mema ni lugha ya Kibinadamu na ya kiulimwengu inayopedeza, na kwa lugha hiyo Maswahaba na wafuasi wamefahamiana na mataifa waliokuwa na mawasiliano nao, kwa sababu ya hayo watu wameingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi, na jambo lililo muhimu sana ni kwamba ruwaza njema inalazimika kuheshimu itikadi.

 

Print
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.