Udugu wa Manabii na Uislamu wa kimataifa (4)

  • | Thursday, 26 October, 2017
Udugu wa Manabii na Uislamu wa kimataifa (4)

     Mahitaji ya Uislamu wa kimataifa
Hakika Uislamu wa kimataifa unawajibisha juu ya wafuasi wake wawe na sifa kadhaa, na miongoni mwa sifa hizo zifuatazo:
1.    Waislamu ni lazima wadhihirishe ruwaza njema katika mwenendo wao kwa kulinda heshima ya kibinadamu, kama kisa kilichotokea katika enzi ya Umar Ibn Al-Khattab wakati mtoto wa Amr Ibn Al-Aas mtawala wa Misri alipokataa kulipizwa kisasi wakati alipompiga mkristo mmisri juu ya uso wake, wakati huo Umar Ibn Al-Khattab akasema "lini mmewalazimisha watu wawe watumwa na ilhali mama zao wamewazaa wakiwa huru?".
2.    Kutekeleza utumwa kwa Mwenyezi Mungu peke yake, na kuwaokoa watu kutoka kuwaabudu wanadamu; hakika Uislamu Umemwokoa mwanadamu aliyepotea mbali na njia ya uongofu kuelekea njia iliyo bora zaidi, nayo ni itikadi ya Tawheed isiyojua mola isipokuwa Mwenyezi Mungu: {Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu}, [Aal-Imraan:64].
3.    Kumsaidia mdhulumiwa na kumnusuru mnyonge na kuwalinda wawili hao na kuwapa haki zao kutoka anayewadhulumu.
Qurani imejaalia kutetea haki ya waliodhulumiwa na wanyonge ni miongoni mwa kazi za waislamu wote, na kutokana na hayo imeainishwa sura kamili katika fiqhi inayoitwa "Bab Al-Siyaal" kuhusu kumtetea mdhulumiwa -sio kulinda damu yake tu, bali heshima na karama-, na fiqhi ya kiislamu inaona kwamba mwislamu akikataa kutetea haki za mdhulumiwa kwa mujibu wa aya za Qurani na hadithi za Mtume (S.A.W), basi atachukua dhambi na atastahiki kuadhibiwa.
Na miongoni mwa aya hizo: {Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako}, [Al-Nisaa:75], na kauli yake Mwenyezi Mungu: {Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayoyafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapokodoka macho yao}, [Ibrahiim:42]
Na hayo yote yamedhihiri katika hotuba ya kwanza ya Abu Bakr Al-Siddiiq alipochaguliwa Khalifa ya waislamu, akasema:
"Ama baada, kwa hakika nimeshachaguliwa niwe mtawala wenu japokuwa mimi si aliye bora zaidi miongoni mwenu, na jueni kwamba mwenye nguvu ni dhaifu mbele yangu mpaka nichukue haki ya mdhulimiwa kutoka kwake, na dhaifu ni mwenye nguvu mbele yangu nimpe haki yake".

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.