Dalili na hoja zinazozuia kumkufurisha mwislamu (1)

  • | Saturday, 28 October, 2017
Dalili na hoja zinazozuia kumkufurisha mwislamu (1)

     Baadhi ya wasomi wanaofuata Ahlul-Sunna wanaona kwamba madhehebu sahihi ni: imani inayokuwa mchanganyiko kati ya itikadi na utendaji kazi, na kwamba kukiri hakutoshi katika kuhakikisha imani, na mtazamo huu tukiuzungumzia ni lazima tuuzingatie kuwa ni rai tu, na sio madhehebu miongoni mwa madhehebu na kwamba ni ya kweli, na dalili za kisheria hazisisitizi tu kwamba mtazamo wa Uislamu -kuhusu kwamba imani ni kukubali kwa moyo, na utendaji kazi ni sharti yake-, bali dalili hizo zinasisitiza kwamba haijuzu kwa mtu yeyote kuwakufurisha watu hata zikiwa amali zao chache sana, kwani tukifanya hivyo itakuwa fujo kubwa, na ardhi itaharibika, na inajulikana kwamba kuna kauli nzuri na msingi kwa kila anayetaka kupambana na wanaobeba utamaduni wa kukufurisha- inasema: "haikutolea kutoka imani isipokuwa unapokanusha uliyoyaamini hapo kabla", na kauli hii imesisitizwa na dalili na hoja, na labda wakufurishaji watambue kauli hii vizuri ili wanajiweka mbali na mawazo hayo potovu, na zifuatazo ni baadhi za dalili juu ya hayo:
Mwenyezi Mungu anasema: {Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa hak},[Al-Hujurat:9], na hapa tunaangalia kwamba ukweli wa imani umetinganisha na ukweli wa utendaji kazi; maana ingawa mauaji ni miongoni mwa madhambi makuu, isipokuwa Mwenyezi Mungu anawaita wauwaji hao "waumini", na kuna dalili nyingine; Mwenyezi Mungu anasema: {hakika walioamini na wakatenda vitendo vizuri}… katika aya kadhaa, hivyo Mwenyezi Mungu ameunganisha baina ya utendaji kazi na imani, pia katika dalili ya tatu Mwenyezi Mungu Anasema akimzungumzia Mtume wake (S.A.W): {Kama Mola wako Mlezi alivyokutoa nyumbani kwako kwa Haki, na hakika kundi moja la Waumini linachukia. Wanajadiliana nawe kwa jambo la Haki baada ya kwisha bainika, kama kwamba wanasukumwa kwenye mauti nao wanaona}, [Al-Anfaal:5,6].
Na dalili ya nne kauli yake Mwenyezi Mungu: {Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?}, na dalili ya tano kauli yake Mwenyezi Mungu: {Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache(, hivyo Mwenyezi Mungu amewaita waumini ingawa wao wamejitia uzito katika ardhi, na hii bila shaka ni dhambi kubwa; kwani hawataki kwenda kupigana vita pamoja na Mtume (S.A.W), na kuna dalili nyingi sana katika Qurani zinzosisitiza kwamba mtendaji madhambi au dhambi kuu  sifa za imani haziondoshwi kutoka kwake, je kuna anaye elimu zaidi ya hayo?.....


D. Abdelminiim foad

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.