Dalili na hoja zinazozuia kumkufurisha mwislamu (2)

  • | Monday, 30 October, 2017
Dalili na hoja zinazozuia kumkufurisha mwislamu (2)

     Hakika dalili na hoja zinazozuia kumkufurisha mwislamu ni wazi sana na zinachukuliwa kutoka Qurani na Sunnah ya Mtume (S.A.W) na kutoka urithi wa kale wa Uislamu ulio safi sana, na kufuatia yaliyotangulia kutajwa kutoka dalili za Qurani zinazozuia kumkufurisha mwislamu, tunataja dalili na hoja kutoka Sunnah kuhusu uharamu wa kumkufurisha mwislamu.
Na katika Sunna takatifu kuna usisitizo kuhusu uharamu wa kumkufurisha mwislamu katika hadithi nyingi, na miongoni mwake ni kauli yake (S.A.W) katika Sahihul-Bukhari na Muslim, imepokewa kutoka kwa Ibn Umar, kwamba Mtume (S.A.W) amesema "mtu yeyote akisema kwa nduguye: "Ewe Mkafiri" basi dhambi ya hayo huwa juu ya mmoja miongoni mwao akiwa mkweli katika kauli yake hiyo, au itampata mwenyewe"  na hadithi hii inafunga mlango wa kukufurisha, ambao wenye misimamo mikali wanajaribu kuingia kwenye mlango huo kwa njia zote.
Bali katika hadithi tukufu kuna tishio na adhabu katika siku ya qiyama inayongoja kila anayejaribu kuwashutumu waislamu kwa sababu wa amali zao, au kuwatolea kutoka eneo la imani, -na kuna hadithi inayoeleza kwamba Mtume (S.A.W) Alikuwa hakufanya uadui pamoja na wanaoswali, wala hatafuti yaliyomo nyoyoni mwa watu- bali kuna hadithi sahihi iliyopokewa kutoka kwa Thabit Al-Dahhak "na anayemwita mwamini ewe mkafiri, basi ni kama kumwua".
Na kuna hadithi nyingi zinazosisitiza juu ya udharura wa kutowepo haraka katika kuwakufurisha watu, na kwamba wanachuoni wakubwa wa umma wameshadidia sana juu ya udharura wa kupambana na wakufurishaji, na kufedhehesha kauli zao, na kusifu elimu yao kwa upotovu kamili….


D. Abdelminiim foad

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.