Imamu Mkuu Alaani shambulio lililolengea Msikiti wa Al-Rawda mjini Areish

  • | Saturday, 25 November, 2017
Imamu Mkuu Alaani shambulio lililolengea Msikiti wa  Al-Rawda mjini Areish

     Imamu Mkuu wa Al-Azhar Profesa; Ahmed Al-Tayyib alaani kikali shambulio la kigaidi lililolengea msikiti mmoja wa mtaa wa Bi'r Al-Abd mjini Areish, akisisitiza kuwa ugaidi unataka kuwaathiria wamisri vibaya na kuwalazimisha wasipambane nao lakini ugaidi huo utashindwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na utashi wa wamisri wanaojitahidi kumaliza na kushinda balaa hiyo wakiwa pamoja.
Al-Azhar Al-Shareif na Imamu wake Mkuu walaani sana lile shambulio la kigaidi la kikatili lililolengea msikiti wa Al-Rawda mjini Areish, Sinai kaskazini likasababisha kuuawa kwa mashahidi zaidi ya mia mbili na majeruhi makumi wengine, hapo ndipo Imamu Mkuu anasisitiza kuwa kumwaga damu za wasio na hatia, kuvunja heshima ya nyumba za Mwenyezi Mungu, kuwahofisha wanaosali na wasio na kosa ndiko ufisadi katika ardhi, jambo linalostahiki upambano mkali zaidi dhidi ya wahalifu hao wanaotaka kuharibu nchi na kuwatishia watu wake sawa waislamu misikitini au wakristo makanisani, kwa hiyo inabidi kupambana na magaidi hao wasiotambua kiwango cha chini mno cha maadili ya kibinadamu wakakwenda kinyume na maumbile sawa wakawa wakatili zaidi kuliko wanyama.

Image


Imamu Mkuu ametilia mkazo kwamba inapaswa kusahdidisha mapambano dhidi ya makundi haya ya kigaidi kwa kuzuia misaada ya kifedha, silaha, wapiganaji kufika kwa magaidi hao.
Imamu Mkuu ameashiria pia kwamba magaidi baada ya kuyalengea makanisa wakaanza kulengea misikiti, jambo linalothibitisha kuwa magaidi hao hawana imani wala msingi yoyote ya kidini wala hawana ila uharibifu na kufanya maangamizi katika ardhi pasipo na kutofautiana baina ya mwislamu na asiye mwislamu, mkubwa na mdogo, mwanamume na mwanamke, wanajeshi, polisi, wananchi wa kawaida, bali wanalengea kueneza vurugu na uharibifu ardhini. Akiongeza kwamba ugaidi huo huwafanya wamisri wawe pamoja zaidi ambapo hatima yao ni moja waislamu na ndugu zao wasio waislamu, lakini ugaidi huo utashindwa hatimaye na wamisri ndio watakaoshinda kwa kushikamana na kuwa pamoja.

Image


Vile vile, Imamu Mkuu amesisitiza kuunga mkono kwake na kwa Al-Azhar Al-Shareif na wamisri wote kwa mamlaka ya nchi ikiongozwa na Jeshi na Polisi katika juhudi zao kupambana na ugaidi huo na kuwaangamiza wanamgambo hao wa kikatili na kuiokoa nchi kutoka shari na jinai zao. Akimwombea Mwenyezi Mungu Awakubali mashahidi na kuzituliza nyoyo za jamaa wao na kuwanemeeshea wajeruhiwa kwa kupona haraka.

 

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika


 

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.