Daesh: Jihad ni faradhi inayopaswa kupitishwa juu ya waislamu wote....

  • | Saturday, 2 December, 2017
Daesh: Jihad ni faradhi inayopaswa kupitishwa juu ya waislamu wote....

Daesh: Jihad ni faradhi inayopaswa kupitishwa juu ya waislamu wote, nayo inawajibika kuwaua wasio waislamu wote wakitoa dalili kwa kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W): "Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu".  

    Aya hiyo imehusiana na washirikina wa Makkah, na maana ya aya hii ni: "Na piganeni nao ili mwislamu yeyote asipatwe na fitina katika dini yake na ili mwislamu asidhulumiwa, na kwa ajili ya kumkinga mwislamu asibadilishe itikadi yake kutoka imani kwenda ukafiri", na amri ya kupigania vita hapa ilikuwa katika hali  ya kujitetea na kuzuia uadui uliofanywa na washirikina dhidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) na mwaswahaba wake (R.A.), bali zaidi ya hayo hakika anayefuatilia na kusoma vyema vita vya Mtume wa Mwenyezi Mungu huona kwamba vita hivyo vyote vilikuwa kwa sababu ya kimantiki inayokubaliwa na akili, na vita vyote vilikuwa kwa ajili ya kutetea, kuzuia uadui na kulinda ulinganio na waislamu katika nchi zao, hayo yote hayakutajwa katika hotuba za Daesh kamwe, na hata wanamgambo wa Daesh hawakutaja kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W): {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua}. {Al-Anfal:61}, na pia wamesahaulika kimakusudi kauli ya Mwenyezi Mungu: {Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu}. {Al-Mumtahina:8}, na kwamba aya hizo mbili ni aya zinazohusiana na mapigano yote yanayotokea baina ya waislamu na wasio waislamu wakati wote  na mahali pote.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.