Katika taarifa ya haraka baada ya Swala ya Ijumaa Imamu Mkuu kwa wenyeji wa Al-Quds: Mapinduzi yenu yawe kwa kiwango cha imani yenu kwa suala lenu...

  • | Friday, 8 December, 2017
Katika taarifa ya haraka baada ya Swala ya Ijumaa Imamu Mkuu kwa wenyeji wa Al-Quds: Mapinduzi yenu yawe kwa kiwango cha imani yenu kwa suala lenu...

Katika taarifa ya haraka baada ya Swala ya Ijumaa
Imamu Mkuu kwa wenyeji wa Al-Quds: Mapinduzi yenu yawe kwa kiwango cha imani yenu kwa suala lenu, upendo wenu kwa nchi, na sisi tuko pamoja nanyi wala hatutawapuuzeni

 

  Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Krehemu
Al-Azhar Al-Shareif imefuatilia kwa masikitiko makubwa ule uamuzi unaotolewa na mamlaka ya Marekani kwa kuutangaza mji wa Al-Quds Al-Shareif kama mji mkuu wa utawala wa kizayuni dhalimu katika hatua isiyotanguliwa na mfano na ukikukaji ulio dhahiri kwa mikataba ya kimataifa na upuuzaji wazi kwa hisia za waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu, pamoja na mamilioni ya wakristo waarabu ambao wameafikiana na ndugu zao waislamu juu ya kuyatakasa misikiti ya kihistoria na makanisa mjini humo.

Image

 

Kwa hakika, Al-Azhar Al-Shareif kwa niaba ya ulimwengu wa kiislamu mzima inakataa kabisa uamuzi huo batili, pia tunasisitiza kwamba kuchukua uamuzi kama huo ni udanganyifu wazi na uchafuo mkubwa kwa historia na uharibifu kwa mustakbali wa mataifa ambao haikubalika kukaa kimya bila ya kuwa na jibu la haraka na lenye hekima madamu waislamu wako hai.
     Wote watambue kuwa Al-Quds ndio mji mkuu wa Palestina, nchi iliyokaliwa na mamlaka dhalimu ya kizayuni, wala hatutakubali suluhisho jingine, na taharuki yoyote ya kimataifa isiyokiri ukweli huo, basi haitakubaliwa bali itasababisha hatima mbaya zaidi.

Image

 

  Tunaonya kikali hatari ya kushikilia uamuzi huo batili ambao unachocheza fitina na kukuza hisia za chuki nyoyoni mwa waislamu na nyoyoni mwa wanaotaka kupitisha amani duniani, na unatishia sana usalama na amani ya kimataifa.
Watawala wa Marekani wanapaswa kutambua vyema kwamba siasa ya kuupendelea upande mmoja, kutokuwa na uadilifu, kuwaunga mkono wakaliaji wa kizayuni madhalimu, kuzipora haki za mataifa na mabaki yao ya kikale, na kuziporomosha staarabu zao ndiyo siasa isiyoambatana na misingi ya ustaarabu wa kibinadamu, kwa hivyo siasa kama hii haitadumu kabisa, bali itashindwa haraka au baadaye, na suala la uarabu wa Al-Quds litabaki ndilo suala la waarabu na waislamu lililo muhimu zaidi kabisa ambalo halitasahaulika kamwe.
   Sisi hapa nchini Misri; nchi ya Al-Azhar, Uarabu na Uislamu.. tunawaombea Viongozi wa nchi za kiislamu, Serikali zake, Jumuiya ya nchi za kiarabu (A.L.), Shirika la Ushirikiano wa kiislamu, na Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ya haraka kwa ajili ya kuondosha uamuzi huo na kuufuta kabisa.
 Vile vile, tunawaombea pande husika zote miongoni mwa mashirika ya kimataifa na taasisi za kuchangia kueneza amani na kuimarisha usalama duniani na kupigana na siasa za ukaliaji zachukue taratibu za lazima na za haraka ili kumaliza tatizo hilo baya la kimataifa na la kibinadamu.
Pia, tunatoa wito kwa mataifa wa ulimwengu wa kiarabu na kiislamu kukataa mikakati hiyo inayoandaliwa na wazayuni na wamarekani, na kujirudisha uelewa ulio sawa kuhusu suala la Al-Aqsa ambao ni Msikiti Mtakataifu wa tatu na Qebla ya kwanza na mahali pa matembezi ya Mtume wetu Mohammed (S.A.W.) Mtume wa mwisho kabisa.
Mwishoni, tunawaambia ndugu zetu huko Al-Quds: "Tunaheshimu sana ushujaa wenu usio na mfano, tukizaunga mkono juhudi zenu za ukombozi, na mapinduzi yenu ya tatu yawe kwa kiwango cha imani yenu kwa suala hilo, upendo wenu kwa nchi, na sisi tuko pamoja nanyi wala hatutawapuuzeni, Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui .."
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa} Al-Israa: 21.

Ijumaa 8/12/2017
Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.