Imamu Mkuu akataa kumpokea makamu wa Trump akisisitiza: inapaswa kufuta aumuzi huo usio wa kisheria na unaolengea kupoteza haki za wapalestina kuhusu mji mkuu wa nchi yao "Al-Quds"

  • | Saturday, 9 December, 2017
Imamu Mkuu akataa kumpokea makamu wa Trump akisisitiza: inapaswa kufuta aumuzi huo usio wa kisheria na unaolengea kupoteza haki za wapalestina kuhusu mji mkuu wa nchi yao "Al-Quds"

    Katika taharuki ya kihistoria Mheshimiwa Imamu Mkuu wa Al-Azhar Profesa Ahmed Al-Tayyib amekataa ombi la makamu wa rais wa Marekani Donald Trump kukutana naye mwishoni mwa mwezi huu, akabainisha ghadhabu na kukataa kwake kwa ule uamuzi dhalimu wa mamlaka ya Marekani kwa kuutangaza mji wa Al-Quds (Jerusalem) uwe mji mkuu wa utawala wa kizayuni na kuhamisha ubalozi wa Marekani nchini Israel kwenda mji huo, jambo linalozingatiwa uchochezi mbaya kwa hisia za waislamu ulimwenguni kote.
Inatajwa kwamba Mike Pence makamu wa rais wa Marekani Donald Trump alikuwa ameomba kukutana na Imamu Mkuu kipindi cha ziara yake nchini Misri iliyopangwa kufanyika tarehe 20 mwezi uliopo, na Ubalozi wa Marekani mjini Kairo ulikuwa umepanga mkabala wa Pence na Imamu Mkuu kwenye makao makuu ya Sheikhi wa Al-Azhar wiki iliyopita na yule Mheshimiwa Imamu Mkuu alikubali mwanzoni, lakini baada ya tangazo batili lililotolewa na rais wa Marekani kuhusu kuutambua mji wa Al-Quds kama ni mji mkuu wa mamlaka ya kizayuni, basi Imamu Mkuu ametangaza kukataa kwake kufanyika kwa mkutano huo akisisitiza kuwa: "Al-Azhar Al-Shareif haiwezekani kuambatana na wanaochafua na kubadilisha historia na kupora haki za mataifa wakifanya ukiukaji mbaya dhidi ya maeneo matukufu pao"

Image

 

     Imamu Mkuu ameongeza akisema: "Inakwaje, nikutane na waliowapa wasiyoyamiliki kwa wasiostahiki, na rais wa Marekani anatakiwa kuondoa uamuzi huo haraka kwani ni uamuzi batili kisheria"
Vile vile, Imamu Mkuu ametuhumia rais wa Marekani na mamlaka wake kuhusika kuchocheza fitina na hisia za chuki nyoyoni mwa waislamu, bali nyoyoni mwa wanaounga mkono kueneza amani na kupitisha usalama ulimwenguni kote, na pia amewatuhumu kupoteza maadili na misingi ya kidemokrasia na kuzivunja nguzo za uadilifu na amani, zile nguzo na yale maadili wanayoyahitaji sana wananchi wa kimarekani na mataifa wote duniani, akitilia mkazo kuwa rais wa Marekani kwa uamuzi wake huo amechangia kueneza chuki na kuimarisha migongano, ambayo Al-Azhar Al-Shareif inafanya juhudi kubwa mno kwa ajili ya kuyamaliza na kupambana nayo wakati wote, na ikijitahidi kueneza usamehevu na upendo baina ya watu wote.
 Inakumbukwa pia kuwa Imamu Mkuu amewahotubia wenyeji wa mji wa Al-Quds leo baada ya swala ya Ijumaa, akawaombea kuwa na ushujaa wa kutosha kwa kiwango cha upendo wao kwa nchi yao na mji mkuu wake Al-Quds Al-Shareif, akisisitiza kuwa Al-Azhar Al-Shareif inaunga mkono wapalestina mbele ya uamuzi dhalimu huo.
Al-Azhar Al-Shareif ilikuwa imetangaza msimamo wake thabiti tangu mwanzo wa kupitisha uamuzi wa mamlaka ya kimarekani kukiri kuwa Al-Quds (Jerusalem) ndio mji mkuu wa utawala wa kizayuni na kuamua kuhamisha ubalozi wa Marekani kwenda mji huo, ikionya sana kuhusu matokeo mabaya na hatima hatari za uamuzi huo ambao unaweza kusababisha matatizo mengi yanayoweza kuathiria vibaya amani na usalama wa kimataifa.

Image

 

Ijumaa 8/12/2017
Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.