Uislamu hauruhusu kuwaua watu wasio na hatia

  • | Monday, 18 December, 2017
Uislamu hauruhusu kuwaua watu wasio na hatia

     Bila shaka dini ya kiislamu ni ya uadilifu na uwastani, amani na usuluhi, upendo na ucha Mungu. Na Uislamu umeipa nafsi ya kibinadamu cheo cha juu. Na kwa kuzingatia kwamba kumuua mwanadamu ni uhalifu mkubwa usioridhika na Allah na mtume wake na dini zote za mbinguni na Vitabu Vitakatifu vilivyoteremshwa na Allah juu ya mitume wake, Kwa hivyo basi, tunawaombea watu wote wanaofuata sharia zote za mbinguni wasiuane wala kumsaidia mwuaji yeyote wala kushirikiana katika mauaji mwanadamu yeyote pindi akiwa mwislamu au asiye mwislamu, kama ilivyokuja katika Qurani Tukufu: “Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu”.{Al-Maida: 2}.  
     Kutokana na yote hayo, Uislamu hauruhusu kumuua mtu yeyote asiye na hatia kwa baadhi ya makosa ya jinai. Hivyo, kama Mwislamu yeyote ataua mtu asiye na hatia, Mwislamu huyo ametenda dhambi baya kabisa, na hakika tendo hilo haliwezi kufanywa kwa jina la Uislamu. Mwenyezi Mungu Anasema: “Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Amekataza isipo kuwa kwa haki, Na aliyeuliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa”.{Al-Israa 33}. Vile vile, Mwenyezi Mungu Amesema: “Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke, na Tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane, Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi, Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabar”.{ Al-Hujuraat:13}
     Na tukiangalia kwa macho ya uadilifu hali ya mataifa ya kiafrika yanayoishi chini ya utawala wa makundi ya kigaidi, hasa Afrika magharibi ambapo kundi la Daesh la Afrika (Boko Haramu) lipo, na Afrika Mashariki ambapo kundi la Al-Shabab lipo, tunakuta kwamba wasio na hatia sawa wakiwa wanaume au wanawake, wazee au watoto wachanga, wanauliwa, wanatishwa, wanatekwa nyara, wanabakwa, na makazi yao yanachomwa, mambo yasiyoafikiana na akili na dini.
     Hakika jinai na mambo ya mauaji yanayofanywa na kundi la kigaidi la Boko Haramu dhidi ya walio salama huko Afrika Magharibi ndio ushahidi mkubwa juu ya tunayoyasema. Kundi hilo lilisonga mbele makundi ya kikatili zaidi duniani, kwa kuwa mashambulizi yake yanalenga maeneo yanayojazwa na watu kama masoko na misikiti hasa katika sala ya Al-Fajiri na Ijumaa, mbali na kutumia mabomu, vifaa vya kulipua na mikanda ya vifaa vya kulipuka, ambayo huongeza idadi ya wafu na wajeruhiwa.
     Kuhusu kundi la Al-Shabab huko Afrika Mashariki,  wote wanaafikiana kuwa ni kundi la kigaidi linalotaka kumeza Somalia na kuzuia nafasi zote za utulivu na maendeleo nchini humo, na katika eneo lote la Afrika mashariki, na linatumia njia zote za kigaidi za vitendo vya mauaji, kutekwa nyara, kukata shingo, Kupiga mawe hadi kufa dhidi ya watu wasio na hatia.
     Mwishoni, tunataka kusema kwmba Uislamu ni dini ya usawa na salama, na sheria ya kiislamu ina shime kubwa ya kulinda maisha ya mwanadamu na uadui wo wote. Katika Qurani Tukufu, Uislamu umesifu kuihuisha nafsi na kulaani kuiua, M.Mungu Anasema: “Aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote”.{ Al-Maidah: 32}.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.