Taarifa ya Imamu Mkuu kuhusu kuupokea Mwaka Mpya wa 2018

  • | Tuesday, 9 January, 2018
Taarifa ya Imamu Mkuu kuhusu kuupokea Mwaka Mpya wa 2018

     Akielezea Matamanio yake kwa Mwaka Mpya uwe na Kheri na Amani, Imamu mkuu: mwaka wa 2018 uwe mwenye uadilifu na usamehevu.. Kujibu Mahitaji ya wanaonyimwa na dhalili.
Mheshimiwa Imamu mkuu sheikh wa Al-Azhar profesa Ahmad Al-Tayyeb, Raisi wa Baraza la Wakuu wa Waislamu anaeleza matamanio yake kuhusu mwaka wa 2018 uwe na amani na kheri kwa wanadamu wote, akihimiza kwa ulazima wa kufanya juhudi za kueneza utamaduni wa usamehevu, na kuishiana pamoja duniani kote na kukataa sura zote za ubaguzi, ya fikra kali na ya ugaidi.
Pia, imamu mkuu anasisitiza juu ya ulazima wa kufanya kazi pamoja ifikayo mwanzoni mwa mwaka mpya ili kueneza uadilifu na usawa, na kushirikiana sote katika kujibu Mahitaji ya wanyonge, waliopotezwa na waliodhulumiwa duniani kote.
Aidha, Imam anasisitiza juu ya kuwa majaribio ya miaka iliyopita, na hata matukio ya kihistoria ya zamani na ya hivi karibuni, zinasisitiza kwamba amani na ustawi wa ubinadamu hazikubali kutenganishwa, na kwamba haiwezekani kuwepo kwa sehemu yeyote ulimwenguni ambayo inaneemeka kwa ustawi na amani wakati ambapo sehemu zingine kuna watu wanaoteseka na fujo na kunyimwa, jambo linalohitaji jamii ya kimataifa na nguvu zake zenye kuathiri zifanye juhudi kubwa ili watu wote ulimwenguni waishi bila ya njaa, umaskini na utenganisho. kwa hivyo, masuala ya njaa huku Afrika, ukandamizaji na ubaguzi huko Myanmar pamoja na ukaliaji wa Palestina na majaribio ya kuiba haki za wapalestina na vitakatifu vyao, ni masuala yenye umuhimu zaidi yanayopasa kupata shime kubwa za ulimwengu katika mwaka wake huu mpya.
Pia imamu anamwomba Mwenyezi Mungu ijaalie mwaka mpya ni mwaka wa kutenda kazi, wa utoaji, na kufanya bidii na wa kujitahidi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya nchi yetu Misri inayopendwa na ulimwengu wetu wa Kiarabu na Kiislamu, Na kufanya kazi pamoja ili kuendelea ulimwengu wetu kwa namna inayotufanya kuishi katika amani na usalama, ustawi na mustakbali bora kwa wanadamu wote.

 

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.