Taarifa ya Al-Azhar kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Kunusuru Suala la Al-Quds

  • | Tuesday, 16 January, 2018
Taarifa ya Al-Azhar kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Kunusuru Suala la Al-Quds

Ukiwa na shime kubwa ya kiarabu nay a kimataifa …

Mkutano wa Kimataifa wa Al-Azhar wa kunusuru Al-Quds waanza kwa kutilia mkazo maudhui tatu kuu:

  • Uelewa kwa Suala la Al-Quds
  • Kisisitiza Utambulisho wa Mji Mtakatifu wa Al-Quds
  • Majukumu ya Watawala na Pande Husika kuhusu Suala la Al-Quds

 

Mkutano wa kimataifa wa Al-Azhar kwa ajili ya kunusuru suala la Al-Quds  (Jerusalem), utakaofanyika tarehe 17 na 18 Januari, utajadili pande kuu kadhaa yanayoshughulika kwa kurejesha tena uelewa kuhusu suala la Al-quds (Jerusalem), na kusisitiza utambulisho wake wa Kiarabu na wa Kiislamu, na kubainisha kwa majukumu ya kimataifa kwa mji takatifu unaokaliwa, na kusisitiza kwamba kanuni ya kimataifa inamlazimisha mamlaka  yanayokalia kuhifadhi hali ya kisasa nchini.

Image

Na mkutano wa kimataifa, ulioandaliwa na Al-Azhar Al-Sharief kwa kushirikiana na Baraza la wakuu wa waislamu, utajadili masuala kadhaa kupitia pande tatu, ya kwanza: chini ya anuani ya "utambulisho wa Kiarabu wa Al-quds (Jerusalem) na ujumbe wake", ambapo inakusanya anuani ndogo kadhaa zinazozungumzia "cheo cha kidini na kimataifa kwa Al-quds  (Jerusalem), Al-quds  na ustaarabu wake katika historia na hivi sasa, na matokeo ya kubadilisha utambulisho katika kuenea chuki, na kuyajadili madai ya kizayuni kuhusu Al-quds na Palestina."

Na anuani ya pili ya mkutano ni "kurejesha tena uelewa kwa suala la Al-quds (Jerusalem)", inayozungumzia masuala kama "hali ya kisheria na ya kimataifa kwa Al-quds, na jukumu la kisiasa katika kurejesha tena uelewa, na jukumu la utamaduni na elimu kuhusu  suala la Al-quds, na umuhimu wa jukumu la vyombo vya habari katika kurejesha tena ufahamu".

Image

Na pande la tatu la mkutano litajadili "wajibu wa kimataifa kuhusu Al-Quds", na inazungumzia maudhui kadhaa kuhusu "wajibu wa taasisi za kidini kuhusu Al-quds, na pia "wajibu wa taasisi za kimataifa", na "wajibu wa jamii ya kimataifa na ya kiraia kuhusu suala la Al-quds".

       Na "mkutano wa kimataifa wa Al-Azhar kwa ajili ya kunusuru  Al-quds  ",unakuja katika mfumo wa maamuzi yaliyochukuliwa na  Imamu mkuu Profesa Ahmed Al-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharief na kiongozi wa Baraza la wakuu wa waislamu, kuhusu uamuzi wa kunukuu ubalozi wa Marekani kwa mji wa Al-quds  uliokaliwa, na kudai kwamba ni mji mkuu wa mamlaka dhalimu wa kizayuni.

Na inatarajiwa kwamba mkutano utatoa idadi ya mapendekezo muhimu ambayo yanayoweza kusaidia suala la Palestina, na kuzisisitiza haki za wapalestina kuhusu kuanzisha dola yao yenye huru na mji mkuu wake ni Al-quds, na pia kuhifadhi vitakatifu vya kiislamu na vya kikristo huko mji wa Al-quds, pamoja na idadi kadhaa ya maamuzi na hatua zitakazowasaidia vijana waelewe vizuri suala la Al-quds  na historia yake na vitakatifu vyake.

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali

Kitengo cha Lugha za Kiafrika

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.