Dondoo za Taarifa ya Ufunguzi wa Mkutano wa Al-Azhar kuinusuru Al-Quds

  • | Wednesday, 17 January, 2018
Dondoo za Taarifa ya Ufunguzi wa Mkutano wa Al-Azhar kuinusuru Al-Quds

     Mheshimiwa Imamu Mkuu katika taarifa ya ufunguzi wa Mkutano wa Al-Azhar wa kimataifa wa kuinusuru suala la Al-Quds:
•    Kutoka hotuba yake kwenye kikao cha ufunguzi cha Mkutano wa kimataifa wa Al-Azhar kwa kunusuru Suala la Al-Quds, Imamu Mkuu:
•     Kwa hakika Mkutano wetu unatoa tahadharisho na kuhimiza juhudi za kulitetea suala la Al-Quds dhidi ya usaliti wa mamlaka dhalimu ya kizayuni.
•    Nadokeza kutambua mwaka huu wa 2018 kama ni mwaka wa Al-Quds Al-Shareif kupitia kueneza uelewa ulio kamili kuhusu suala hilo na kuwaunga mkono watu wa mji huu mtukufu.
•    Bila shaka ukaliaji wowote haudumu milele, bali inakuja siku ya kuondosha ule ukaliaji dhalimu, ingawa inaonekana kwamba hilo ni jambo gumu wakati mwingine, lakini hatima ya kila dhalimu haitakuwa ila kushindwa na kufeli katika mikakati yake yanayolengea kuwatesa watu na kuwanyima haki zao.

•    Sisi ni walinganiaji wa amani na usalama unaotegemea uadilifu na kutimiza haki, hasa zile haki zisizokubali kupuuzwa, na haiwezekani kuomba haki kama hizo kwa kujidhalilisha au kuacha sehemu yoyote kutoka nchi na mahali patakatifu.
•    Ukweli unaosikitisha sana ni kwamba mitalaa yetu haikusanya mada inayoshughulikia kuunda uelewa kuhusu suala la Palestina kijumla na suala la Al-Quds hasa.
•    Tunayoyakosa kwenye mitalaa yetu ya kimafundisho na pia katika vyombo vya habari ni kuzungumzia suala la Al-Quds kwa urefu na kwa makini ili tutambue ukweli wa suala, tusitosheleka kupokea habari au ripoti za kawaida.
•    Kwa hakika uamuzi dhalimu wa Raisi wa Marekani kwa kuutambua mji wa Al-Quds kama ni mji mkuu wa mamlaka dhalimu ya kizayuni, inapaswa kukabiliwa na taharuki za kiarabu na kiislamu zinazosisitiza sana Uarabu wa mji huu mtukufu na kukataa kila linalopingana na ukweli huo.
•    Wakuu wa Ummah miongoni mwa watawala, wahubiri, wasomi na wengineo, wanatakiwa kutanabahi kuwa ummah huu unalengwa kupatwa na mashaka na hata kuangamizwa kabisa, na kwamba lazima tuhifadhi dini yetu, utambulisho wetu wa kiarabu, mitalaa ya kimafundisho na ya kimalezi na pia umoja wa mataifa wake na kuishi kwao pamoja kwa amani.   


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.