Katika ziara yake ya kwanza barani Afrika… Mheshimiwa Imamu Mkuu afanya ziara nchini Senegal na Nigeria kwa lengo la kuimarisha maadili ya amani na kueneza mawazo ya kukubaliana

  • | Tuesday, 10 May, 2016
Katika ziara yake ya kwanza barani Afrika… Mheshimiwa Imamu Mkuu afanya ziara nchini Senegal na Nigeria kwa lengo la kuimarisha maadili ya amani na kueneza mawazo ya kukubaliana

Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu katika kipindi cha siku chache zijazo ataanza ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu kushika madaraka ya kuendesha Al-Azhar Al-Shareif ambapo atazuru nchi mbili za Senegal na Nigeria.
Ziara hiyo inapewa shime kubwa ambapo Mheshimiwa Imamu Mkuu atakutana na Maraisi wawili wa Senegal na Nigeria na mawaziri wakuu wa nchi hizo mbili na pia baadhi ya wahusika wakuu nchini humo, vile vile atafanya nishati na mikutano kadhaa kwa ajili ya kuimarisha maadili ya amani, kueneza fikira za mazungumzo na kusameheana na kuishi pamoja kwa amani, na pia kusisitizia dhana sahihi za dini, na uwastani wa Uislamu na kukataa vurugu na ugaidi, licha ya kufanya mikutano mikubwa na vijana ili kuwaonya kutoka hatari za mawazo batili na kuwakinga dhidi ya wito za ukatili na misimamo mikali.
 Inatazamiwa kwamba Mheshimiwa Imamu Mkuu katika ziara yake hiyo nchini Senegal na Nigeria atatoa hotuba kwa mataifa wa bara la Afrika hasa na waislamu wote duniani kwa ujumla, pia atatoa muhadhara mbele ya wanavyuoni wakubwa na wahusika wengi na watu wa jamii za huko.
Ziara ya Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu inapewa shime kubwa mno katika pande tofauti za kirasmi na katika vyombo vya habari.

 

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.