Ziara ya Imamu mkuu Kwa Ureno

  • | Friday, 16 March, 2018
Ziara ya Imamu mkuu Kwa Ureno

     Mheshimiwa Imamu Mkuu Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharief profesa Ahmad Altayib Rais wa  baraza la wakuu wa waislamu ameondoka  ‎Misri asubuhi ya jumatano 14 machi, akifanya ziara ya nje inayokusanya nchi mbili "ureno na Muritania", ambapo Mheshimiwa  atakutana na wahusika wakuu wa nchi mbili, na kushiriki katika mikutano kadhaa yenye umuhimu.
Wakati wa ziara yake nchini Ureno, Mheshimiwa Imamu Mkuu ‎atakutana na Rais wa nchi, Mkurugenzi mkuu wa Bunge, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje. Pia atatoa hotuba katika sherehe itakayofanyika kwa mnasaba wa kumalizika miaka 50 ya kuanzisha jumuia ya kiislamu mjini Lishbona kwa hudhudhuria Rais wa Ureno na Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa. Chuo kikuu cha kikatholiki – kinachozingatiwa chuo kikuu kikubwa zaidi nchini Ureno -   kitafanyika  sherehe ya kumkaribisha  Imamu mkuu, naye atatoa hotuba kwa ajili ya  mnasaba huo.
Baada ya kumalizika ziara yake nchini Ureno,   Mheshimiwa Imamu Mkuu sheikh wa Al-Azhar ‎Al-Sharief ataelekea nchini Muritania; kwa ajili ya kushiriki katika semina na wataalamu wakubwa wa dini nchini Muritania kuhusu kukabiliana na hali ya vurugu na siasa kali .Pia Imamu Mkuu atakutana na Rais wa Muritania, Mkurugenzi Mkuu wa Bunge, Waziri Mkuu, wanachouni wakubwa  na watu wakuu wa nchi, na Mheshimiwa atashuhudia kutia saini idadi ya mikataba ya ufahamiano kati ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar na taasisi kadhaa za kitaaluma nchini Muritania.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.