Tuhuma ya kuhalalisha kumwua asiye mwislamu

  • | Friday, 31 August, 2018
Tuhuma ya kuhalalisha kumwua asiye mwislamu

     Kundi la Daesh limezitegemea dalili zifuatazo kutoka Qurani Tukufu ili kuhalalisha kuwaua wasio waislamu na kila anayehitilafu nao.

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema :{ Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu}. (Al-Baqarah: 193)

Mwenyezi Mungu Amesema: {Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia}. (Al-Tawbah: 4)

 

Jibu:

Uislamu ni dini ya kimataifa inayohimiza amani, kuziheshimu dini zote na kuharamisha kumwaga damu, na kwa kuzichambua dalili zinazotegemewa na kundi hilo la kigaidi, tutaona kuwa wanakata aya kutoka muktadha yake, na wanaitumia katika mahali pengine wakisahaulika aya zilizo kabla na baada ya aya hiyo, kwa mfano wanategemea kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina} kama ni dalili ya kuhalalisha kuwashambulia wasio waislamu chini ya jina la Jihadi bila ya kuangalia aya iliyoitangulia, ambapo Mwenyezi Mungu amesema: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui} aya hiyo inabainisha kwamba mapigano hayakuruhusiwa  isipokuwa kwa ajili ya kulinda nafsi dhidi ya maadui, na sio kwa ajili ya kuwashambulia watu.

Mwenyezi Mungu Amesema {wala msianze uadui}, na Uislamu haukuja kwa ajili ya kuwalazimisha watu waufuate, Mwenyezi Mungu amesema: {Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae}, bali amri inahusiana na (ahadi na mikataba) uliofanyika baina ya Waislamu na Wasio Waislamu, na rai ya Wasio Waislamu kuhusu ahadi na mikataba hiyo, na jambo hilo limethbitishwa na aya za Qurani, lakini kwa sharti ya kutokata aya kutoka muktadha yake, hivyo imetubidi tuangalie vizuru aya zilizo kabla na baada ya aya hizo zinazotegemewa na kundi hilo.

Hakika sheria imewagawanya wasio waislamu kuhusu kufanyika mikataba kwa aina sita:

Kwanza: wasio waislamu waliopewa ahadi na hawakushambulia waislamu:

Aya zote zimekuja zikibeba uhuru wa itikadi na uhuru wa kufuata dini yoyote, Mwenyezi Mungu Amesema: {hakuna kulazimisha katika dini}(Al-Baqarah:256), {Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?}(Yunus:99), {Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari}, (Qaaf:45), {Wewe si mwenye kuwatawalia}, (Al-Ghashiyah:22), { Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae} ([Al-Kahf:29), {wala msianze uadui} (Al-Baqarah:190).

Pili: wasio waislamu hawakupewa ahadi na wamewashambulia wengine:

Kauli yake Mwenyezi Mungu: { Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui. Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipokutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri. Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu}, (Al-Baqarah:190,193). Na amri ya kwanza ilikuwa kwa kusamehe na kuvumilia maudhui, kisha Mwenyezi Mungu ameruhusu kutetea ili washambuliaji wasimamishe uadui wao katika kauli yake: {Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia} (Al-Hajj:39), kisha imekuja katika sura ya Al-Tawbah aya inayoamuru kuwauwa kila waliovunja ahadi yao uliofanyika pamoja na Mtume (S.A.W), amri hiyo kwa kuua ilikuja kama adhabu juu ya kuvunja ahadi yao na kwa kutowasameh hata wakisimamisha mashambulizi yao isipokuwa wakitubu na wakasimamisha swala na wakilipa zaka.

Tatu: wasio waislamu waliopewa ahadi na hawakushambulia lakini hawakutekeleza, na wakajaribu kuwaridhisha waislamu kwa midomo yao ilhali nyoyo zao zinakataa kataa, basi kauli ya Mwenyezi Mungu inawajumuisha: { Itakuwaje iwepo ahadi na washirikina mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake}, na kauli yake: {Itakuwaje! Nao wakikushindeni hawatazami kwenu udugu wala ahadi. Wanakufurahisheni kwa midomo yao tu, na nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wapotovu. Wamenunua thamani ndogo kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakazuilia watu na Njia yake. Hakika hao ni maovu waliyokuwa wakiyatenda}, na kauli yake: { Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yaokwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini. Wala wasidhanie wale walio kufuru kwamba wao wametangulia mbele. La, wao hawatashinda. Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari}, maana msiwashambulie kwa farasi , bali {ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua}, na kauli yake: {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu}, na kuli yake: {Basi wakitubu na wakashika Sala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazichambua Aya kwa watu wajuao}.

Nne: wasio waislamu waliopewa ahadi na wakatekeleza

Mwenyezi Mungu Anasema: {Isipokuwa washirikina ambao mliahidiana nao kisha wasikupunguzieni chochote, wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi hao watimizieni ahadi yao mpaka muda wao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha-Mungu}, (Al-Tawbah:4), na kauli yake: {ila wale mlioahidiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu wanakwenda nanyi sawa, nanyi pia nendeni sawa nao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu},

katika kauli yake: {Itakuwaje iwepo ahadi na washirikina mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake, ila wale mlio ahidiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu wanakwenda nanyi sawa, nanyi pia nendeni sawa nao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu. Itakuwaje! Nao wakikushindeni hawatazami kwenu udugu wala ahadi. Wanakufurahisheni kwa midomo yao tu, na nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wapotovu. Wamenunua thamani ndogo kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakazuilia watu na Njia yake. Hakika hao ni maovu waliyo kuwa wakiyatenda. Hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi; basi hao ndio warukao mipaka}, basi wasio waislamu wote waliofanya ahadi pamoja na Mtume (S.A.W) walikuwa baina ya waliokataa kutekeleza ahadi yao wakitangaza kukataa kwao, na baina ya waliojificha wanaowaridhisha waumini, lakini nyoyo zao zinakataa.

Tano: wasio waislamu waliopewa ahadi kisha wakavunja ahadi yao pamoja na Mtume (S.A.W).

Basi kauli ya Mwenyezi Mungu imewajumuisha: {Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu}, (Al-Tawbah:5).

Sita: wasio waislamu walioahidi kisha wakavunja ahadi yao pamoja na waumini baada ya kufa kwa Mtume (S.A.W).

Basi kauli ya Mwenyezi Mungu inawajumuisha: {Na wakivunja viapo vyao baada ya kuahidi kwao, na wakatukana Dini yenu, basi piganeni na waongozi wa ukafiri. Hakika hao hawana viapo vya kweli. Huenda (kwa hayo) wakaacha}, maana kama hawakutubu na wala hawakuvunja ahadi basi: {Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari}.

Mwenyezi Mungu Amesema: "Basi mnapowakuta waliokufuru wapigeni shingoni mwao" basi hukumu hiyo inawahusu waislamu wanaopigana na makafiri katika uwanja wa mapigano, basi hao wameamriwa kuwapiga maadui pigo za kuuwa, na hukumu hiyo inakuwa wakati wa vita tu, ama vita ikiisha basi mwislamu hana haki ya kuanza uadui wake au kumwua mmoja wa makafiri akikutana naye pamoja na kupata nafasi ya kumwua. Basi heshima ya asiye mwislamu imehifadhiwa, na damu yake imeharamishwa kumwagiwa, haijuzu kwa mtu kumdhuru, kwani ni jengo la Mwenyezi Mungu na yeye ndiye peke yake aliyemleta hapa duniani na akamjaalia kuwa khalifa yake, na kwa sababu hiyo akaihifadhi damu yake.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.