Kituo cha habari cha AL ـAzhar AL- SHARIF: Imamu mkuu Hakuashiria kamwe kukataa au kuharimisha kuwaoa zaidi ya mwanamke mmoja

  • | Saturday, 9 March, 2019
Kituo cha habari cha AL ـAzhar AL- SHARIF: Imamu mkuu Hakuashiria  kamwe  kukataa au kuharimisha  kuwaoa zaidi ya  mwanamke mmoja

     Kituo cha habari cha AL‎ـAzhar AL- SHARIF‎ kimefuatilia yaliyonukuliwa  na baadhi ya mitandao ya kieliktronika na mitandao ya kijamii kuhusu kipindi cha tarehe 1 mechi 2019 A.D. cha Programu ya  "Mazungumzo ya shekhi wa AL ‎ـAzhar" katika  Kituo cha Satellite cha Misri, na  yaliyomo katika kipindi hiki kuhusu suala la " kuwaoa zaidi ya  mwanamke mmoja".
Na kituo kinasisitiza kwamba mheshimiwa Imamu mkuu Hakuashiria  kamwe kukataa au kuharimisha kuwaoa zaidi ya mwanamke mmoja, ‎bali mheshimiwa  ‎alisema kabla ya hapo katika hotuba yake katika mkutano wa Fatwa ya kiulimwengu, tarehe 17/10/2016 A.D: "Ninaanza kusema kwamba mimi siombi sheria zile zinazofuta haki ya  kuwaoa zaidi ya  mwanamke mmoja, bali ninakataa sheria yoyote inayobinga na sheria za Qurani Tukufu au sunna iliyotahiriwa, au inayozigusa kwa njia ya kidogo au kikubwa; ili niwazuie watu wanaosema maneno yasiyokweli na kuyaweka mbali na uhakika wake,  wale wanafanya hivyo kwa ajili ya kufaidika na kupata fedha kupitia hayo. Lakini mimi ninajiuliza: jambo lolote linalomfanya mwislamu maskini kumwoa mwanamke mwengine – kwa mfano - na anaacha mke wa kwanza na watoto wake wa kiume na wa kike wanateswa na umaskini na upotevu, wala hana inayomzuia kutumia haki hii ya kisheria, na  kuenda mbali na makusudio yake na malengo yake.
Mazungumzo yote ya mheshimiwa katika kipindi hicho yalikuwa kuhusu fujo ya kuwaoa zaidi ya  ‎mwanamke mmoja  na kufasiri aya tukufu inayohusiana na suala hilo, na kwamba aya hii inaweka sharti ya uadilifu baina ya wanawake, pia mheshimiwa amejibu juu ya wanaozingatia kwamba kuwaoa zaidi ya  ‎mwanamke mmoja‎ ni asili ya kuwaoa.‎

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.