Al-Azhar yalaani mashambulizi ya kigaidi juu ya misikiti miwili Nizolanda.. na inasisitiza: kiashirio hatari cha kuzidika hotuba ya chuki na Islamophopia

  • | Friday, 15 March, 2019
Al-Azhar yalaani mashambulizi ya kigaidi juu ya misikiti miwili Nizolanda.. na inasisitiza: kiashirio hatari cha kuzidika hotuba ya chuki na Islamophopia

     Al-Azhar Al-Sharif pamoja na Imamu yake mkuu profesa/Ahmad Attayib; Shekhi wa Azhar inalaani mashambulizi mabaya ya kigaidi yaliyolenga misikiti miwili mjini "Christchurch" huko Nizolanda, wakati wa kutekeleza Sala ya ijumaa, ambayo yamesababisha kuua na kujuruhiwa makumi, ikitahadharisha kuwa mashambulizi hayo yanazingatiwa kiashirio hatari juu ya matokeo mabaya yanayotokana na kuzidika hotuba ya chuki na kuwafaniya wageni ni maadui na kueneza Islamophopia katika nchi kadhaa za ulaya hata ile iliyokuwa ikijulikana kwa kuishana pamoja na wakazi wake.

Al-Azhar Al-Sharif inasisitiza kuwa mashambulizi hayo yanayopita kiasi cha uharamu wa nyumba za Mwenyezi Mungu na kumwaga damu zilizoharamishwa, yanapaswa kuwa  kionyo cha tahadhari ya kutotendeana kwa upesi na makundi ya kibaguzi yanayofanya vitendo  kama hivyo vya kichuki, na kuwa ni lazima kufanya juhudi kubwa zaidi za kuimarisha maadili ya kuishi pamoja na kusameheana baina ya watu wa jamii moja, bila ya kutazama dini zao na tamaduni zao.

Al-Azhad Al-Sharif inatoa mkono wa upole kwa familia ya mauaji, ikimwombea Mwenyezi Mungu Mtukufu Awarehemu na kuwaingiza peponi, na kuwatia watu wao subira,   na kuwaneemisha waliojuruhiwa waponye haraka.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.