Katika ziara yake ya kwanza barani Afrika… Leo..Mheshimiwa Imamu Mkuu aondoka akielekea Abuja.. ambapo atafanya mazungumzo na Rais wa Nigeria njia za kupambana na mawazo makali

  • | Monday, 16 May, 2016
Katika ziara yake ya kwanza barani Afrika… Leo..Mheshimiwa Imamu Mkuu aondoka akielekea Abuja.. ambapo atafanya mazungumzo na Rais wa Nigeria njia za kupambana na mawazo makali

Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu, atasafiri hivi leo jumatatu akielekea mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ambapo inatazamiwa kwamba atakutana na Rais wa Nigeria Muhammad Bukhari kwenye ikulu jijini humo ili kujadiliana kuhusu njia za kupambana na mawazo makali.
Pia inatazamiwa kwamba ziara hiyo itashuhudia mikutano kadhaa vile vile mikutano na nishati kadhaa zikiongozwa na mkutano na makamu wa rais, pamoja na kukutana na wanachama wa baraza kuu la masuala ya kiislamu nchini Nigeria na wakubwa wa maulamaa wa nchi hiyo, vile vile Mheshimiwa yule atakutana na baadhi ya mabalozi wa nchi za kiislamu kule Nigeria.
Zaidi ya hapo Mheshimiwa Imamu Mkuu atatoa hotuba kwa mataifa wa bara la Afrika na waislamu wote duniani kutoka kituo kikuu cha kimataifa cha mikutano katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ambapo maulamaa wakuu na idadi kubwa ya wakubwa wa wahusika na watu wa jamii watahudhuria, hotuba ile itakuwa kwa anuani ya:
"Uislami ni dini ya amani…changamoto za kupambana na mawazo makali na ugaidi".
Mheshimiwa Imamu Mkuu ataambatanishwa katika ziara hii na ujumbe wa hali ya juu nao ni: profesa; Ali Al-Nieemy, katibu mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu, Kadhi; Mohammad Abdul-Salam, mshauri wa Sheikhi mkuu wa Al-Azhar, profesa; Ibrahim Al-Hud-hud mkuu wa Chuo kikuu cha Al-Azhar na profesa; Abu Zeid Al-Amir mkuu wa idara kuu ya taasisi za Al-Azhar.
Ziara ya Imamu Mkuu kwenda Nigeria ambayo ni ziara ya kwanza ya Imamu Mkuu tangu aliposhika madarakani, inakuja katika juhudi za Al-Azhar Al-Shareif kwa kushirikiana na baraza la wakuu wa waislamu kwa ajili ya kuimarisha maadili ya amani na kueneza fikira ya mazungumzo, kusameheana, kuishi pamoja kwa amani, kusisitiza dhana sahihi za dini, na kutilia mkazo uwastani wa Uislamu na kukataa kwake kwa vurugu na ugaidi.
Ziara ya Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu nchini Nigeria inapewa shime kubwa mno katika pande tofauti za kirasmi na katika vyombo vya habari.

 

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.