Akipokelewa na mapokezi na mazingatio kubwa ya kirasmi na kitaifa …. Imamu Mkuu awasili mji mkuu wa Nigerea Abuja ... Kesho atoa hotuba kwa mataifa wa bara la Afrika

  • | Monday, 16 May, 2016
Akipokelewa na mapokezi na mazingatio kubwa ya kirasmi na kitaifa …. Imamu Mkuu awasili mji mkuu wa Nigerea Abuja ... Kesho atoa hotuba kwa mataifa wa bara la Afrika

Kabla ya muda chache, Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu, amefika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ambapo inatazamiwa kwamba atakutana na Rais wa Nigeria Muhammad Bukhari kwenye ikulu jijini humo ili kujadiliana kuhusu njia za kupambana na mawazo makali.
Mheshimiwa Imamu mkuu  na ujumbe mwenye kuambatana naye walipofika wamepokewa na idadi ya wakubwa wa wahusika nchini humo, na sheikh Ibrahim Saleh Al-Husiny Mufti wa Nigeria, na balozi Ashraf Abdul Qadir Salama balozi wa Misri huko Nigeria, na idadi ya Viongozi wa makundi ya Kidini.
Kesho siku ya Jumanne, Mheshimiwa Imamu Mkuu atatoa hotuba kwa mataifa wa bara la Afrika na waislamu wote duniani kutoka kituo kikuu cha kimataifa cha mikutano katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ambapo maulamaa wakuu na idadi kubwa ya wakubwa wa wahusika na watu wa jamii watahudhuria, hotuba ile itakuwa kwa anuani ya:
"Uislami ni dini ya amani…changamoto za kupambana na mawazo makali na ugaidi".

Mheshimiwa Imamu Mkuu ataambatanishwa katika ziara hii na ujumbe wa hali ya juu nao ni: profesa; Ibrahim Al-Hud-hud, Mkuu wa Chuo kikuu cha Al-Azhar, profesa; Abu Zeid Al-Amir mkuu wa idara kuu ya taasisi za Al-Azhar, profesa/ Abdul Fatah Al-Awary, Mkuu wa kitivo cha Usul Addin, na Kadhi; Mohammad Abdul-Salam, mshauri wa Sheikhi mkuu wa Al-Azhar
Ziara ya Imamu Mkuu kwenda Nigeria ambayo ni ziara ya kwanza ya Imamu Mkuu tangu aliposhika madarakani, inakuja katika juhudi za Al-Azhar Al-Shareif kwa kushirikiana na baraza la wakuu wa waislamu kwa ajili ya kuimarisha maadili ya amani na kueneza fikira ya mazungumzo, kusameheana, kuishi pamoja kwa amani, kusisitiza dhana sahihi za dini, na kutilia mkazo uwastani wa Uislamu na kukataa kwake kwa vurugu na ugaidi.

 

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.