Dondoo za hotuba ya Imamu Mkuu wa Al- Azhar katika Bunge ya Ujerumani (Bundestag)

  • | Wednesday, 16 March, 2016
Dondoo za hotuba ya Imamu Mkuu wa Al- Azhar katika Bunge ya Ujerumani (Bundestag)

•    Tunashukuru msimamo wa kibinadamu wa mshauri "Merkil" unaohusiana na waliokimbia adhabu ya vita na maangamizi yake huko Mashariki wala hatusahau kusifu mwelekeo wake kuhusu Islamufobia aliposema: Uislamu ni sehemu ya Ujerumani.
•    Mimi sina mwelekeo wo wote wa kisiasa au kichama wala sifuati itikadi yo yote yenye kuambatana na siasa ya mwelekeo wa kulia au wa kushoto.
•    Mimi nafanya juhudi kubwa kupitisha amani kwa watu wote, wakiwa wa nchi, jinsi na taifa tofauti, hata wakihitilifiana katika dini, itikadi na madhehebu.
•    Imamu Mkuu kwa Waislamu wa Ulaya: nyinyi ni sehemu ya ulimwengu wa kimagharibi, basi mshikamaneni na mafundisho ya Uislamu na usamehevu wake.
•    Sasa Maulamaa wa Al Azhar wanajitahidi kupambana na mawazo mabaya pahala po pote duniani, yale mawazo yanayogeuza mafundisho ya Kiislamu ili kusaidia kukuza fitina jambo linalosababisha umwagaji damu na kuharibu nchi.
•    Al-Azhar Al-Shareif na baraza la wakuu wa Waislamu wanatuma misafara ya amani duniani ili kusahihisha mawazo yenye makosa yasiyoambatana na mafundisho ya Uislamu pamoja na kuwatahadharisha vijana wawe mbali na mawazo makali.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.