Taarifa ya baraza la Wakubwa wa Waislamu kuhusu ukiukaji wa kizayuni dhidi ya Msikiti Mtakatifu wa Al-Aqsa na kujaribu kufaradhisha mgwanyiko wa kiwakati na kimahali juu yake

Alhamisi: 23 Dhul-Hijja 1436 H.J / 8, Octoba, 2015 B.K.

  • | Saturday, 10 October, 2015

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, shukrani zote kwa Mungu, swala na amani ziwe juu ya Mtume wa Mungu na familia yake na maswahaba wake na wanaomfuatilia
Kwa hakika "Baraza la wakubwa wa waislamu linafuatilia kwa wasiwasi maendeleo ya hali inayajiri hivi karibuni mjini Al-Quds na msikiti wa Al-Aqsa, ambayo ni  ukiukaji ulio wazi unaofanywa na wazayuni katika nyua za msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa, hasa matendo ya kiadui yanayofanywa na askari wa Israel tangu 23 – 8 – 2015, ambayo ni uikuaji wazi kwa maadili ya kibinadamu na misingi ya kidini, isitoshe bali ni uikuaji wazi kwa misingi ya sheria ya kimataifa, na maamuzi yote ya kimataifa, pia ni uikuaji wazi dhidi ya uhuru wa kuitekeleza ibada uliomo katika Azimio la Haki za Binadamu iliyopitishwa na Umoja wa Mataifa,  kwa namba ya (217) kwa mwaka 1948.
"Baraza la wakubwa wa waislamu" linaamini kwamba matendo hayo yote na mazoezi ya kijinai ni sehemu ya mpango wa kubadilisha utambulisho wa mji wa Al-Quds, mpango uliowekwa hapo zamani, na uliojitokeza wazi kupitia kwa hatua za kuchukua umiliki wa eneo kubwa zaidi la ardhi za wapalastina ili kujenga hali mpya ya Jiografia ya kisiasa ya mjini, na pia kupitia ujenzi wa makazi ya wakaliaji wa kiyahudi na kuwahamisha wakazi wa kiasili ili kupitisha halisi mpya  katika idadi ya wakazi na maeneo ya kuishi kwao, na kusababisha ukosefu wa usawa wa idadi ya wakazi katika mji wa Yerusalemu, ili kutakuwa wengi wa wakazi wake ni wakaliaji wa kiyahudi chini ya ulinzi wa jeshi ya Israel.
Katika suala hili, Baraza la wakubwa wa waislamu linalaani mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya msikiti wa Al-Aqsa, Qiblah ya kwanza na miongoni mwa maeneo matatu matakatifu zaidi katika Uislamu, ambayo yalizidi katika siku za hivi karibuni kupitia kwa uvamizi wa msikiti wa Al-Aqsa na mashirika ya kiyahudi yenye msimamo mikali kwa msaada na ulinzi wa jeshi ya  kizayuni, ambayo imewarahisisha kuingia viwanja vya msikiti huo ili wauvunje na kuuvamia na kufanya ukiukaji wa ndani yake,  na kufunga kwa barabara za msikiti na kunajisiwa sehemu takatifu na Jeshi la Israel, na kutowaruhusia Waislamu kuuingia kwa nyakati ndefu, na kuwazuia kutekeleza haki yao ya kidini na ya kihistoria kuhusu msikiti wa Al-Aqsa ambao ni sehemu halisi ya ibada inayohusu Waislamu pekee wala haikubaliki iwe mahali pa pamoja panapoweza kushirikiana au kugawanywa kwa namna yo yote.
Vile vile, Baraza la wakubwa wa waislamu linalaani vikali shughuli za kuchimba zinazofanywa chini na kuzunguka mwa msikiti wa Al-Aqsa kwa dai la Hekalu la Sulemani wanalolidai mayahudi.
Na Baraza la wakubwa wa waislamu linauombea umma wa Kiislamu na jamii ya kimataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kufanya kazi ili kuzuia kubadilisha  utambulisho wa mji wa Al-Quds ukawe wa kizayuni, na kujaribu kuipindua alama za Kiislamu na Kikristo mjini humo, na kuwalazimisha waislamu na wakristo walio ni wenyeji asili wa mji wa Yerusalemu waache makazi yao.

Pia, Baraza la wakubwa wa waislamu linawaombea waislamu wote wazingatie kabisa suala la Yerusalemu Al-Quds na kufanya bidii ili kuokoa msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa na kuzuia uharibifu makusudi wa kinyama na mashambulizi kizayuni yanayolengea kuuharibu au kunajisi uwanja na vifaa vyake wa msikiti huo.

Mwishoni, Baraza la wakubwa wa waislamu linawatakia jamii ya kimataifa kuzuia Israel kufanya matendo mabaya hayo, na umuhimu wa kulazimika kwa mamlaka hiyo ya kizayuni kwa sheria za kimataifa na maazimio ya kimataifa zlizotolewa kuhusu suala hili.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.