Katika ziara yake kwa Ukumbi wa Kihistoria wa Amani mjini Monester …. Imamu Mkuu wa Al- Azhar: Amani baina ya mataifa hutegemea mazungumzo baina ya dini

  • | Thursday, 17 March, 2016
Katika ziara yake kwa Ukumbi wa Kihistoria wa Amani mjini Monester …. Imamu Mkuu wa Al- Azhar: Amani baina ya mataifa hutegemea mazungumzo baina ya dini

Katika ziara yake kwa Ukumbi wa Kihistoria wa Amani mjini Monester ….
Imamu Mkuu wa Al- Azhar: Amani baina ya mataifa hutegemea mazungumzo baina ya dini


Kwa kuitika mwaliko wa mkuu wa mji wa Monester nchini Ujerumani…Mheshimiwa Imamu Mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif Profesa; Ahmad Al-Tayyib, mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu alifanya ziara kwa Ukumbi wa Kihistoria wa Amani ambao ulishuhudia kusaini azimio la amani la kumaliza vita vya kimadhehebu hapo mwaka 1648 B.K. Imamu Mkuu alipokelewa na Mkuu wa mji wa Monester Livy Markous, askofu Hanz Yashki mkuu wa tume ya mazungumzo baina ya dini mbali mbali, mkuu wa Chuo Kikuu cha Monester na viongozi kadhaa wa kanisa na kiraia mjini humo.
Mwanzoni mwa mkutano huu, Mkuu wa mji wa Monester alimkaribisha Mheshimiwa Imamu mkuu akielezea furaha yake kwa ziara hiyo kwa mji na ule Ukumbi wa Kihistoria, akisisitiza kwamba ziara hii ni ziara ya kihistoria itakavyotajwa na kukumbukwa milele, pia alitoa wito kwa kuanza mazungumzo ya amani baina ya dini kutoka mji huu wa amani.
Na katika hotuba yake mbele ya waliohudhuria, Mheshimiwa Imamu Mkuu alisisitiza kwamba kuna udharura wa kufanya juhudi za pamoja kwa ajili ya kusimamisha vita na mizozo yanayoendelea ulimwenguni, akitilia mkazo kuwa amani na usalama baina ya mataifa inategemea sana mazungumzo baina ya dini akibainisha kwamba Uislamu na Ukristo ndizo dini za amani na upendo.
Na baada ya kumaliza hotuba yake hii, Mheshimiwa Imamu Mkuu Profesa; Ahmad Al-Tayyib Sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif, mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu aliandika ibara katika daftari ya kihistoria ya kusajili zaiara, iliyopo ukumbini humo akiambataniwa na kupiga makofi kwa wingi kutoka waliohudhuria ambao walimkaribisha sana yule Mheshimiwa na wajumbe waliokuja naye.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.