Hotuba ya Imamu Mkuu wa Al- Azhar katika Bunge la Ujerumani (Bundestag)

  • | Wednesday, 16 March, 2016
Hotuba ya Imamu Mkuu wa Al- Azhar katika Bunge la Ujerumani (Bundestag)

Ewe Profesa; Norbert Lamert mkuu wa bunge la Ujerumani
Enyi Mabibi na Mabwana waheshimiwa wabunge wa Bundestag
Enyi watukufu mlio hadharani!
Assalamu Alykuma Warahmatu Allahi Wabarakatuh
Mwanzoni mwa hotuba yangu tafadhali nipe ruhusa ya kueleza shukrani zangu kwenu kwa kunipa nafasi ya kuwepo hapa na kutoa hotuba kwenu na kwa wajerumani wenye kuheshimiwa kupitia kwenu enyi hadhira na wabunge.
Nina furaha kubwa mno kwa kuwepo hapa kwenye Bundestag bunge la kihistoria ambalo lilikuwa shahidi juu ya matukio ya kihistoria yaliyoleta mageuzi makubwa katika historia ya Ulaya. Na vipi bunge hilo lilifanikiwa kawasaidia wajerumani wavuke matatizo yao ya kisiasa, kiuchumi na ya kijamii na wakaweza kuanzisha nchi imara inayotajwa kama ni mfano mzuri wa kuiga katika maendeleo yanayotegemea maadili ya uhuru, uadilifu na usawa.
Kwa mnasaba huu naeleza shukrani na maamkizi mema kwa Mshauri Bibi/ Anjela Merkil, na natoa heshima kubwa kwake kwa naiba ya Al-Azhar Al-Shareif msimamo wake wa kibinadamu kuhusu wanaume, wanawake na watoto waliokimbia maangamizi ya vita yanayojiri katika nchi za kimashariki, japokuwa baadhi ya mashaka yanayoweza kumkabili bibi huyo mheshimiwa lakini hakusita kuwasaidia wakimbizi hao katika msimamo bora zaidi ambayo utakumbukwa vizuri sana, inakumbukwa kwamba Al-Azhar ilitolea taarifa ya kumshukuru Mshauri Merkil kutokana na misimamo yake mzuri kuhusu Uislamu na waislamu alipojiunga katika maandamano mjini Berlin kwa kushutumu Islamofobia na akashikamana kwa ushujaa mkubwa ibara ya rais wa zamani wa Ujerumani Christian Volv: "Hakika Uislamu ni sehemu ya Ujerumani"
Na naomba ruhusa kutoka kwenu enyi wabunge! Kujitambaulisha mbele yenu kama ni mtu mwislamu aliyejihusisha na kusoma Uislamu, akaufahamu kama alivyotaka Mwenyezi Mungu kutoka waja wake, na kama alivyoufikisha Mtume wake Mohammad (S.A.W.) … na kwa kweli sina uhusiano wo wote na chama cho chote cha kisiasa au mwelekeo wo wote wa kifikira na wala sijiungi na upande wo wote wa kimawazo sawa wa kulia au wa kushoto, au upande wo wote wa kisasa mwingineo, na wala sina hamu ya kufanya hivyo, sawa kimawazo au kimatendo, lakini mimi ni mwislamu anayependa wanadamu wote, ninajishughulikia sana masuala ya amani kwa namna zake zote kidini, kijamii na kimataifa, na natafutia amani hiyo nikitamani ienea baina ya watu wote bila ya kujali nchi zao, jinsi zao, uraia wao, dini zao, itikadi zao au madhehebu zao.
Enyi Mbibi na Mabwana waheshimiwa!
Sikukuja kwenu kwa kutoa mawidha wala kwa kuusifu Uislamu mbele yenu, lakini nimekuja kwa ajili ya kuhotubia uadilifu wenu kuhusu kuunusuru dini hiyo inayostahiki kutetewa kutokana na dhuluma na tuhuma batili zilizoufikia, ilhali dini yenyewe haina dhambi yo yote kulingana na dhuluma na tuhuma hizo, kwa sababu ya matendo ya wachache wa wanaojiunga nayo, walioufahamu dini hii kimakosa wakautangulia kwa watu kama ni dini ya kumwaga damu inayofanya uadui dhidi ya ubinadamu na kuziharibu staarabu.
Dini hiyo - kama mnavyojua enyi mabwana - ni dini inayofungamana kabisa na dini za mbinguni, ambapo sisi waislamu tunaamini kwamba Taurati, Injili na Qurani ni vitabu vya kuwaongoza watu kwenye njia iliyonyooka, na kwamba kilichokuja baadaye kati yake kinakisadikisha kilichotangulia, na imani yetu kwa Qurani au Mohammad (S.A.W.) haitakamilika ila tukiamini vitabu hivyo vya mbinguni na kwa Mussa na Isa na manabii waliowatangulia (A.S.), tunasoma katika Qurani Mtukufu kauli yake Mwenyezi Mungu: "Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika" Al-Baqarah: 62.
Na sio sahihi yanayosemwa kuhusu Uislamu kwamba ni dini ya mapigano au dini ya kutumia upanga, ambapo tamko hilo la "Upanga" halitajwa katika Qurani hata kidogo…waislamu huamini kwamba Mwenyezi Mungu amemtuma Mohammad (S.A.W.) ili awe sababu ya kuwarehemu malimwengu yote, na sio kwa kuwarehemu waislamu tu, bali alitumwa kama ni rehema kwa wanadamu, wanyama, vitu visivyo uhai na mimea, ilikuja katika Qurani: "Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote" Al-Anbiyaa: 107, naye Mtume Mohammda (S.A.W.) alijisifu akisema: "Kwa kweli mimi ni rehema iliyotuzwa", na ye yote anayefahamu mafundisho nabii huyu bila ya kujali msingi wa kwamba yeye ni rehema kwa ujumla na amani ya kimataifa basi ni mjinga hajui wala hatambui nabii mtukufu huyo wala mafundisho aliyokuja nayo.
Uislamu hairuhusu kupigana na asiye mwislamu kwa sababu ya kukataa kwake kwa Uislamu au dini yoy yote nyingine, ambapo Mwenyezi Mungu kama alivyowaumba waumini aliwaumba pia wengine wasio waumini: "Yeye ndiye aliye kuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda" At-taghabun: 2, na Mwenyezi Mungu hakuwaumba wasio waumini ili atoa amri ya kuwaua na kuwaangamiza, jambo lisilokubalika kiakili na haliafikiani kamwe na hekima ya watu, licha ya hekima ya Mwenyezi Mungu, na uhuru wa kuchagua itikadi ambao umethibitishwa na matini wazi katika Qurani: "Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae" Al-Kahf: 29, na kauli yake (S.W.): "Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu" Al-Baqarah: 256, na imekuja katika katiba aliyoituma Mtume (S.A.W.) kwa watu wa Yemen : "Atakayechukia Uislamu akawa myahudu au mkristo, basi haifai kulazimishwa kuacha dini yake", na historia haina ushahidi hata mmoja juu ya kwamba waislamu waliotawala nchi kadhaa duniani waliwapa wananchi wa nchi yo yote kati ya nchi hizo kuchagua baina ya kujiunga kwa Uislamu au kupigwa na upanga (kuawa), bali walikua wanawapa wakazi wa nchi hizo haki ya kuendelea kufuata dini zao na mila na desturi zao, wala hawakuona dhiki kuishi pamoja nao na kuchanganya baina yao wenyewe kwa wenyewe kupitia ndoa na mahusiano mbali mbali mengine.
Jihad (kupigana vita) katika Uislamu si kupigana kwa ajili ya kupambana na maadui na kujitetea tu, kwani Jihad iliyo kubwa zaidi katika Uislamu ni ile jihad ya nafsi kutoka madhambi na malaghai ya shetani, na inaingia katika dhana ya jihad ya kisheria juhudi yo yote inayofanywa ili kutekeleza maslahi za watu, na juhudi iliyo muhimu zaidi ni ile juhudi ya kupambana na umaskini, ujinga na maradhi, na ya kusaidia anayehitaji msaada, na kuwahudumia watu maskini na kuwasidia, Uislamu haukuwaagiza waislamu kwa kufanya jihad kwa kutumia silaha wala hauwachochea kuifanya ila wakiwa wanajitetea dhidi ya vitendo vya kiadui, na kupambana na vita vya maadui wao, basi hapo ndipo inapaswa kupigana kwa ajili ya kujitetea, na aina hiyo ya jihad imepitishwa katika dini zote, mila na staarabu. Na hiyo si sahihi bali ni kosa kubwa madai yanayosemwa kwamba jihad katika Uislamu ni kubeba silaha ili kuwapigania wasio waislamu na kuwafuatilia kwa ajili ya kuwaangamiza, na la kusikitisha sana kueneza fikira hizo mbaya na maelezo haya yasiyoambatana na maana za kikweli za matini za Qurani na Sunnah kwa lengo la kuituhumu Uislamu na waislamu kwa tuhuma mbaya.
Na sheria ya Uislamu ni sheria inayotegemea misingi ya maadili ya uadilifu, usawa, uhuru na kuhifadhi heshima ya mwanadamu, na Mtume wa Uislamu alitangaza msingi wa usawa baina ya watu katika enzi ambayo akili ya kibinadamu haijawahi kupata uelewa wa kutosha ili itambue ukweli wa msingi huu au kuufahamu, kwani jamii wa wakti huo ulikuwa umejaa utabaka baina ya utumwa na ubwana, japokuwa jambo hilo Mtume Mohammad (S.A.W.) alitoa wito wake wa kihistoria aliposema: "Watu wote ni sawa kama vile ncha za ala ya kuchana", na kaikupita miaka kumi tangu kufariki kwa Mtume (S.A.W.) mpaka alikuja khalifa wa pili Omar Bin Al-Khattab akatoa wito mwingine alipowaombea walii mmoja wa waislamu akimlalamika: "Mbona mmewafanya watu kama ni watumwa ilhali mama zao waliwazaa wakiwa huru".
Nafikiri kwamba nyinyi hapa barani Ulaya kuna kanuni na sheria nyingi zinazoafikiana na sheria za kiislamu - kuhusu uwanja huu - kimatini na kimaana, na hasa hasa zile sheria ambazo zinahusiana na kuhifadhi heshima ya mwanadamu na kumpa uhuru wa lazima, na kutekeleza uadilifu na usawa baina yake na wengineo bila ya kujali dini au madhehemu anazozifuata.
Hapo ndipo nasema kwa waislamu wanaoishi barani Ulaya wakawa ni sehemu mojawapo sehemu za jamii imara ya bara hilo, nawaombea wazingatie maadili hayo ya hali ya juu katika jamii zao ambazo wanaishi ndani yake, na kunufaika kwa jamii hiyo katika kutoa picha nzuri inayofanana na wanayoyaona katika jamii hizo, kuhusu Uislamu na mafundisho yake yenye msamaha, ambayo yanatilia mkazo kuwaheshimu wengine, bila ya kujali dini yake au ukoo wake au taifa lake, na wakumbuke daima kauli yake (S.W.): "Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu" Al-Mumtahinah: 8, na ninapenda sana kwamba kila mwislamu anayeishi barani Ulaya aandike aya hii kwenye mchoro mzuri akauweka juu meza yake au dukani mwake, au juu ya simu yake ya mkononi, akakumbuka wakati wote, kuwa hisani ambayo ni kelele ya adabu pamoja na wazazi, inatakiwa pia wakati wa kutendeana na watu wanaotutendea vizuri wala hawatuudhi, na kwamba uadilifu na kutekeleza ahadi ndiyo tabia ya mwislamu wakati wa kutendeana na ndugu yake mwislamu na pia wakati wa kutendeana na ndugu yake katika ubinadamu.
Ama kuhusu hali ya mwanamke katika sheria ya kiislamu basi yeye ni mshiriki wa mwanaume katika haki na wajibu, na kwa maneno ya nabii wa Uislamu Mohammad (S.A.W.): "Wanawake ni washiriki wa wanaume", wala msidhani enyi mabwana kwamba baadhi ya mateso anayoyapata mwanamke wa mashariki kama vile kumpuuza ni kwa sababu ya mafunzo ya dini, ambapo haya ni madai batili, na yaliyo sahihi ni kwamba mateso hayo yametokana na kujiweka mbali na mafunzo ya Uislamu yanayohusiana na mwanamke, na kupendelea mila na desturi za kikale zisizohusiana na Uislamu kabisa, na kutumia mila na desturi hizo badala ya hukumu zinazohusiana na mwanamke katika sheria ya kiislamu na jamii ya kiislamu ilikosa kufikia mafanikio makubwa tulipokubali  - sisi waislamu - kumpuuza mwanamke na kutozingatia umuhimu wake katika jamii za mashariki.
Enyi Mabibi na Mabwana!
Hakika kuchanganya baina ya watu na kutofautiana kwao ni ukweli ambao Qurani Mtukufu iliputisha, na ikautegemea katika kutunga sheria ya mahusiano ya kimataifa katika Uislamu, nayo ni "kujuana na kutambulishana" ambayo inahitaji kupitisha msingi wa kufanya mazungumzo baina yetu na wanaotuunga mkono na wale wasioafikiana nasi, jambo ambalo tunalihitaji sana ili tuweze kutoka kwenye matatizo ya ulimwengu wa kisasa, kwa hiyo ilikuwa ngumu kwa mwislamu kudhani kuwa watu wote wanatakiwa kufuata dini moja au utamaduni mmoja, kwani matakwa ya Mwenyezi Mungu yamelazimika kuumbwa kwa watu wakiwa tofauti hata katika alama za vidole vyao, Qurani inasema: "Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana" Hud: 118, na anayeamini kwa Qurani hawi na wasi wasi yo yote kwamba matakwa ya Mwenyezi Mungu kuhusu kutofautiana kwa watu hayawezekani kubadilishwa au kugeuzwa na nguvu au ustaarabu wo wote, mumini huyo huzingatia nadharia zinazotamani kuwaunganisha watu katika dini moja au utamaduni mmoja ni nadharia tupu au ni ndoto za utotoni.
Kwa hiyo ikawa la kawaida kwamba Uislamu uliingiliana na wakristo na mayahudi kwa kiwango kinacho wazi, ukaanzisha njia na misingi ya kuishi pamoja kwa amani, mpaka kukubali kufanya ndoa baina ya mwanamume mwislamu na mwanamke mkristo au myahudi hata mke huyu akibakia dini yake baada ya kuolewa na mwanamume mwislamu, na haijuzu kwa mume wake mwislamu kumzuia asiende kanisani au hekalu au kumzuia kufanya ibada zake nyumbani mwa mume wake mwislamu.
Pengine baadhi yenu enyi mabwana wabunge waheshimiwa! Anapinga ninayoyasema, au anajiuliza akikana aliyoyasikia: je, Uislamu na waislamu wakiwa wazuri mno kwa kiwango hicho, basi makundi ya kidini yenye silaha kama vile Daesh na makundi yanayolifanana yalijitokeza vipi kutoka kwa Uislamu na waislamu? Yale makundi yanayowaua wasio na hatia kwa jina la Mwenyezi Mungu, Uislamu na sheria yake? Je, vitendo hivyo vya kikatili visivyofungamani na ubinadamu vinaweza kuharibu kila niliyoyasema kuhusu Uislamu kwamba ni dini ya amani, udugu wa kibinadamu na kurehemu kwa pamoja baina ya watu?
Jibu langu juu ya swali hilo - kifupi - ni: kama dini yo yote miongoni mwa dini za mbinguni ikihukumiwa kutokana na waliyoyafanya baadhi ya wafuasi wake kati ya jinai za mauaji na maangamizi basi dini zote zitatuhumiwa kwa ugaidi na vurugu, kwani magaidi wanaofanya jinai zao kwa jina la dini hawaziwakilishi dini hizo, bali wao - ndio - wahaini wa amana za dini wanazodai kuzifuata na kupigana kwa ajili yake.
Kwa kweli dini zinajitambulisha kupitia kwa mafunzo yake ya kiuungu na kutokana na mawidha ya manabii na mitume waliowasilisha mafunzo hayo kwa watu wakawalingania kuamini kwayo…hivyo hivyo ulikuwa ujumbe wa Bwana wetu Mohammad, na hivyo hivyo ulikuwa ujumbe wa Bwana wetu Isa na Bwana wetu Mussa na jumbe zote za mbinguni kwa watu…
Kisha ugaidi huu ambao sisi sote tunateseka nao siku hizi ulishutumiwa na ulimwengu kote wa kiislamu; maraia, serikali, Al-Azhar, makanisa, vyuo vikuu, wasomi, wenye kutafakuri na wengineo, na tunapaswa sote waislamu na wasio waisalamu kuungana kwa ajili ya kupambana na vurugu, ugaidi na dhuluma kwa namna zake zote, na kufanya juhudi zilizo kubwa zaidi kwa ajili ya kushirikiana katika kumaliza balaa hiyo.
Kwa hakika ugaidi hautofautisha baina ya wahanga wake wakiwa hawafuati mawazo yake ya kikatili wala hawakiri matendo yake, kama baadhi ya wamagharibi wangali dhani kwamba Uislamu unahalalisha jinai za ugaidi basi watu hao lazima wakumbuke kwamba waislamu ndio wanaopata hasara na kulipa gharama ya ugaidi huo kwa damu yao, na sehemu ya miili zao na wake wao na watoto wao kwa marudufu ya hasara wanazozipata wasio waislamu miongoni mwa wahanga wa ugaidi…basi ikwaje kukubali kiakili kuwatuhumia waislamu kwa kuhusiana na wakatili hao ambao Uislamu na waislamu wanawakana.
Na pengine mnaafikiana nami kwamba nchi za mashariki na za magharibi hazina budi kuhusu ugaidi huo ambao unapita mabara nchi hizo hazina budi kufungamana kwa pamoja baina ya dini na wafuasi wake, bali hazina budi kuunda amani baina ya watu wa dini na maulamaa, na mimi naamini kwa nguvu wa tangazo alilolisema mwana wa kiteolojia wa kisasa Hanz Kong ambapo alieleza kwamba: "Haiwezekani kuwepo amani baina ya mataifa madamu hakuna amani baina ya dini" na tangazo hilo hilo lililosemwa na Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Mohammad Mostafa Al-Maraghiy mjini London hapo mwaka 1936 alipoombea urafiki wa kimataifa na maelewano sahihi ya pamoja baina ya ustaarabu wa kimagharibi na ustaarabu wa waislamu.
Enyi mabibi na mabwana naombea ruhusa ya kusema: nilipozungumzia jamii zenu nikishangazwa na siasa zenu ambazo zinategemea misingi ya usawa, demokrasia na kuhifadhi haki za mwanadamu, inawezekana kujitokeza swali la baadhi wakishangaa: kama unayoyasema ni kweli baina ya mataifa ya kiulaya basi hatuoni kitu cho chote kama hiyo katika misimamo kadhaa ya nchi za kimagharibi kuhusu nchi za kiislamu, ambapo wengi wa nchi za mashariki ya kiarabu na kiislamu hawahui lo lote kuhusu nchi za kimagharibi ila siasa ya kutopima kwa usawa, na siasa ya maslahi za pekee ambazo hazijali maslahi za wananchi, wakitoa mifano ya hali hii kwa yaliyotokea kwenye Irak na Libia na nchi nyinginezo, na ujumbe wangu kwenu au matarajio yangu kwenu ni kufanya juhudi kubwa zaidi ili kubadilisha maoni hayo mabaya, na tungeweza kuanza kwa pamoja katika awamu mpya kwa kujitahidi kuimarisha amani wa kimataifa, na kuzima moto wa vita na kusimamisha umwagaji damu na kuwalazimisha wananchi kukimbia nchi zao, na kutatua suala la Palastina kwa suluhisho lililo sawa linalotekeleza amani na utulivu katika eneo. Basi hii mikono yangu nainyosha mbele yenu ili kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kufikia malengo hayo ya kibinadamu … je, kuna atakaejibu?
Enyi Mbibi na Mabwana!
       Kwa kweli demokrasia ambayo tunaitaraji kustawi nchini mwetu za kiarabu na kiislamu, haiwezekani kutekelezwa kwa njia ya vita na mzozo baina ya staarabu na ghasia tupu na mito ya damu na matumizi ya silaha, bali kwa kabadilishana kistaarabu baina yetu nanyi, na mazungumzo ya moja kwa moja, na programu za kubadilishana mafundisho, viwanda na teknolojia.
Na ingawa Al-azhar inashughulikia daima kwa kuboresha hotuba yake na mitaala ya mafundisho yake, lakini Al-Azhar ilifanya huhudi kubwa zaidi kuliko katika kipindi cha miaka ya mwishoni, ikatia mkakati kuu wa kuboresha na kufnaya maendeleo jambo ambalo wakati hautatosha kulieleza kirefu, inatosha mjue kwamba maulamaa wa Al-Azhar wanapambana siku hizi na mawazo ya kimakosa katika mahali po pote, ili kuzuia kuenea mawazo haya mabaya yanayotumia dini katika kuchochea kuzuka fitina ambayo inahalalisha damu na kuharibu nchi, kupitia kwa njia kadhaa zikiwemo kutuma misafara ya amani inayotembea nchi mbali mbali duniani ili kutoa wito kwa amani wa kimataifa, na kukinga bongo za vijana kutoka hatari za ugaidi, na pia kupitia kwa kuanzisha kituo cha Al-Azhar cha uaangalizi kwa lugha za kigeni ambacho kinafuatilia kwa lugha kadhaa na tunataraji kuenea fikira za kuanzisha vituo vinavyofanana nacho ulimwenguni hivi karibuni.
Al-Azhar ilikuwa imefanya mkutano mwezi Desmba 2014 ambapo iliwaita maulamaa waislamu wa kishiia na sunna pamoja na viongozi wa makanisa ya kimashariki na baadhi ya makanisa ya kimagharibi na mwakilishi wa Ayzidiyyiin chini Irak, ambapo mkutano huo ulitoa taarifa yake ya mwisho kwa kuyashutumu makundi ya kigaidi kwa mujibu wa matendo yake ya kikatili na kuwahofisha wasio na hatia yo yote, na kwamba wakristo na waislamu katika nchi za mashariki waliishi pamoja kama ndugu kwa muda wa karne kadhaa na kwamba wote wana hamu ya kuendelea hali hii ya kuishi pamoja kwa amani kwenye nchi inayozingatia usawa na uhuru, na kwanba kuwafanyia wakristo na wengineo maumivu kwa jina la dini ni jambo lisiloafikiana na mafundisho ya kiislamu, na kwamba kuwalazimisha watu waache makazi yao kwa nguvu ni uhalifu tunaoukataa kabisa, na Al- Azhar ilikuwa imewaombea wakristo wabaki nchini mwao mpaka ugaidi huo tunaouteseka nao umalizike.
Na hivi leo Al-Azhar inakataa kabisa kazi zote za kikatili zinazofanywa na wagaidi ambazo Ivory Coast ilikuwa ya mwisho kupatwa na matendo yake maovu, bila ya kusahau kutoa rambi rambi zetu kwa wajerumani kuhusu mhanga wao aliyeuawa katika tukio hilo.

Enyi Mabibi na Mabwana!
Karibu na waislamu milioni ishirini wanaishi barani Ulaya, aghalabu yao wamezaliwa barani humo wakawa wazungu, nasema: watu hawa wote wanapaswa kutendewa kwa usawa baina yao na wananchi asili wa bara hilo, msiwafanye wasikie kwamba ni wahamiaji wasio na umuhimu wo wote katika jamii, wakakosa kujiunga kwao kwa jamii yao, ambapo utiifu kwa nchi ndio kinga iliyo imara ambayo inakinga mtu kutoka upotofu na vurugu.
Kwa kweli mataifa wa nchi za mashariki na kiislamu wanazingatia Ulaya kama ni mshiriki wa karibu mno katika ustaarabu wa bahari ya kati, kwa hiyo mataifa hawa wanakutegemea sana katika kufika ustawi wao wa kimaendeleo yao kielimu, jambo lisilokuwa ila kupitia kwa ushirikiano wa pamoja na kuwaheshimu matakwa ya wananchi katika kuchagua hatima zao na kupanga mustakbali yake.
Nasema tena niliyoyasema hapo juu kwamba A-Azhar ilikuja ili kueleza kuwa iko tayari ya kushirikiana nanyi, na Umoja wa Ulaya...kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya undugu wa kibinadamu na amani ya kimataifa baina ya nchi za mashariki na nchi za magharibi kijumla na kati ya Al-Azhar na wananchi waislamu barani Ulaya ambao nawaombea mwishoni mwa hotuba yangu hii kwenye bunge hilo la kihistoria wajitambulishe kama ni mfano mzuri wa kuiga kwa mwanadamu mwenye kujitakasa anaewakilisha Uislamu na Mtume wake aliyetumwa kama ni rehema kwa walimwengu wote sio kwa waislamu tu..na Al-Azhar iko tayari ya kuandaa mitaala inayoweza kukukinga kutoka mvutano wa makundi yaliyopotea, na inayokusaidia kuwakilisha dini yenu ya kiislamu kwa kuzingatia ndiyo dini iliyo bora zaidi inayofaa kwa maisha ya wakati wo wote na mahali po pote, na mkumbukeni kuwa dini yenu hiyo ilikuwa inatoa mwangaza wake wa kibinadamu na kistaarabu barani Ulaya, jambo ambalo athari zake zingali kuwepo ndani ya vyuo vikuu vya kiulaya mpaka siku tulio nayo hii, na inatosha ushahidi alioutaja mwanafasihi wa kijerumani Gutah na kabla yake wanafasihi na mhakiki wa tamthiliya Leiseng wakisifu Uislamu na ustaarabu wa waislamu..
Nimechukua wakati mrefu lakini nina udhuru ya kwamba nimekujieni nikiwa na tamaa moyoni mwangu, hali yangu kama vile hali ya waislamu bilioni moja na milioni mia saba, tamaa ya kufikia kuishi pamoja kwa amani na mazungumzo ya kistaarabu baina ya nchi za mashariki na za magharibi, nadhani kwamba Bunge hilo linaweza kuchangia vizuri kutekeleza jambo hilo, ambapo linawakilisha wananchi wanaothamini sana uhuru na demokrasia, Bunge ambalo limetufanya tuipa Ujerumani shime kubwa na imani thabiti ya kuwa nchi hiyo inaweza kutusaidia kufikia malengo yetu ya juu kupitia kwa mahusiano yenye ubora wa hali ya juu katika siku zijazo Inshaa Allaah…
    
Assalamu Alykuma Warahmatu Allahi Wabarakatuh

        Ahmad Al-Tayyib
Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.