Hivi leo … Mheshimiwa Imamu Mkuu atoa hotuba ya kimataifa kwa nchi za kimagharibi kutoka Bunge la kijerumani

  • | Tuesday, 15 March, 2016
Hivi leo … Mheshimiwa Imamu Mkuu atoa hotuba ya kimataifa kwa nchi za kimagharibi kutoka Bunge la kijerumani

Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu atatoa leo hotuba ya kimataifa kwa nchi za kimagharibi kutoka Bunge la kijerumani "Bondestag".
Inatarajiwa kwamba yule mheshimiwa atakutana na mkuu wa bunge la kijerumani Bw; Norbert Lamert, vile vile atafanya mjadala wa pamoja na wabunge na mawakilishi wa madhehebu ya kidini na baadhi ya maulamaa na watafiti kuhusu msamaha wa Uislamu kwa anuani ya "Uislamu na Amani"
Mheshimiwa Imamu mkuu alikuwa amefika Jumapili usiku mjini Berlin mji mkuu wa Ujerumani akipokelewa na shime kubwa ya kiserikali na katika vyombo vya habari vya kimagharibi na akiambatana na Mshauri/ Mohammad Abdul-Salam mshauri wa Sheikhi mkuu wa Al-Azhar na Dkt; Mohammad Abdul-Fadeel msimamizi wa kitengo cha lugha ya kijerumani kwenye kituo cha Al-Azhar cha Uaangalizi kwa lugha za kigeni.
 Ziara hiyo ya Imamu Mkuu inakuja katika juhudi kubwa anazozifanya Mheshimiwa Sheikhi mkuu wa Al-Azhar kwa ajili ya kueneza amani katika jamii zote na kujenga mazungumzo ya kimaendeleo baina ya nchi za mashariki na nchi za magharibi kwa kuzingatia heshima ya pamoja na kukubali kwa pamoja, na kuimarisha misingi ya Demokrasia, Uhuru na haki ya mwanadamu kuishi kwa amani.
 

 

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.