Ttarifa ya Al-Azhar El-Sharief kuhusu kuzitukuza huru za kibinadamu

  • | Tuesday, 29 December, 2015

Al-Azhar El-Sharief inayasisitiza yale yaliyotajwa katika maandishi yake kuhusu huru na umuhimu wa kuzitukuza, na miongoni mwake uhuru wa itikadi kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (Hapana kulazimisha katika Dini) na kauli yake (Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu), na inakataa sana yanayofanywa na kundi la kigaidi la Daesh kati ya kuvunja heshima za watu wakiwa waislamu au wasio waislamu kuhusu damu, mali na heshima zao, na Al-Azhar inatangaza kuwa yanayofanywa na kundi hilo kuhusu kuwalazimisha wasio waislamu kufuata dini yao na kuwateka nyara wanawake wao na kuwabaka kwa madai ya kuwa wao ni mateka wa kivita na watumwa, hayahusinai kabisa na Uislamu wala sheria yake iliyo nzuri zaidi, ambapo kuwateka watu na kuwafanyia watumwa kumekwisha na kukamalizishwa na sheria ya kiislamu na kwamba kutekeleza tena utekaji nyara uliofutwa na sheria ya kiislamu ni uhalifu mkubwa wa kidini na kibinadamu. 
Na Al-Azhar Al-Sharief inasisitiza kwamba kundi hilo kwa mujibu wa sheria halimiliki haki ya kutangaza Jihaad, na halimiliki haki ya kuwalazimisha watu kubadilisha dini zao, na hii ni hukumu ya kiujumla ya watu wote, vile vile Al-Azhar Al-Sharief inasisitiza kwamba kumlazimisha mtu yeyote kubadilisha dini yake au kumlazimisha kutamka kwa ulimi wake Shahada mbili au kumlazimisha kuswali na mengineo kati ya mambo yaliyofaradhiswa na Uislamu (hasa ibada), hayo yote hayamaanishi kwamba aliyelazimishwa kufuata Uislamu akawa mwislamu wala haibadilishi itikadi yake, bali yanazingatiwa kuwa uharibifu mkubwa kwa picha ya Uislamu na ukiukaji wa sheria na hukumu zake.
Vile vile Al-Azhar Al-Sharief inasisitiza kwamba kuhalalisha damu, au heshima, au mali za watu wakiwa waislamu au wasio waislamu inazingatiwa ni kukanusha mambo ambayo yamejulikana katika dini kuwa ni dharura (mambo ya kimsingi), na anayefanya hivyo atakuwa amejiweka mbali na mipaka ya dini ya kiislamu.

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.