Al-Azhar Al-Shareif yalaani vitendo vya kiadui dhidi ya waislamu katika nchi za kimagharibi..

  • | Wednesday, 18 November, 2015

Al-Azhar Al-Shareif yalaani vitendo vya kiadui dhidi ya waislamu katika nchi za kimagharibi..ikisisitiza kuwa:

    Serikali za nchi za kimagharibi lazima ziwalinde waislamu na misikiti na mali zao.
    Uchochezi dhidi ya waislamu linaambatana na maslahi za ugaidi.

Al-Azhar Al-Shareif na Imamu wake mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib hueleza kukana kwake kubwa kwa vitendo vya kiadui dhidi ya waislamu wanaoishi nchini za kimagharibi, ambavyo ni pamoja na kuichoma misikiti kadhaa nchini Spain, Uholanzi na Kanada baada ya matukio ya kigaidi mjini Paris, na kupanga kwa baadhi ya vyama vya kulia vyenye misimamo mikali maandamano ambayo yameshuhudia kutangaza ibara mbaya dhidi ya Uislamu na waislamu, na kuchoma nakala za Msahafu Mtukufu, na kuwafukuza waislamu na kuharibu mali zao.

Na Al-Azhar Al-Shareif inasisitiza kukataa kwake kabisa kwa vitendo hivyo vya kibaguzi vinavyopinga yaliyopitishwa na sheria zote za mbinguni, desturi, azimio na mikataba ya kimataifa kwa udharura wa kuheshimu itikadi za wengine na kutofanya ukiukaji kwa vitu vitukufu vyao na mahali pao pa kufanya ibada na mali zao, ikiombea serikali za kimagharibi kuchukua hatua zote za lazima kwa ajili ya kuwalinda waislamu wanaoishi nchini humo kutoka shambulio lo lote wanaoweza kupatwa nalo, na kutochanganya baina ya vitendo vya kundi lililopotea mbali na mafunzo ya dini ya kiislamu ambayo yanaita kwa amani, kusameheana na kuishi pamoja na wengine.

Vile vile, Al-Azhar Al-Shareif inaziombea madaraka husika katika nchi za kimagharibi kuzingatia umakini katika zoezi la kuwafuatilia wahalifu ili kuepukia kuwafanyia wasio na hatia madhara hasa ikijulikana kwamba wasio na hatia wale ni aghalabu ya idadi ya waislamu wanaoishi nchini za kimagharibi, ambao wameingiliana na jamii zao za kimagharibi wakachangia kwa kufanya mafanikio mbali mbali katika nyanja kadhaa, ikionya kwamba baadhi ya maoni makosa kuhusu matukio ya kigaidi ya mwisho na kuyatumia maafa hayo kwa kuchochea dhidi ya waislamu yanasababisha kuzidisha mizozo na matatizo ambayo itasaidia kuukuza ugaidi ambao utafaidika na maoni na chunguzi hizo ili kueneza mawazo na mitazamo mabaya yake.

 

Print
Tags:
Rate this article:
1.0

Please login or register to post comments.