Baraza la wakubwa wa waislamu linashutumu ukiukaji mkubwa wa kizayuni dhidi ya msikiti wa Al-Aqsa …. Na linasisitiza kwamba:
• Matendo ya kizayuni ni ukiukaji wazi kwa maadili za kibinadamu, misingi ya kidini na maazimio na desturi za kimataifa.
• Ukiukaji wa kizayuni ni sehemu ya mpango wa kuufanya mji wa Yerusalemu (Al-Quds) ni mji wa kiyahudi, ulioanza tangu zamani.
• Tunasutumu kazi za kuchimba zinazofanyika chini na kuzunguka kwa msikiti wa Al-Aqsa kwa singizio la kutangaza Hekalu la Sulemani wanalolidai mayahudi.
• Inapaswa kusimamisha matendo ya kuufanya mji wa Yerusalemu (Al-Quds) ni mji wa kiyahudi na kusimamisha kulazimisha kwa wapalastina kuacha makazi yao kwa nguvu.
• Tunawataka waislamu wote wajali na suala la Al-Quds na kuchangia uokoaji wa Msikiti wa Al-Aqsa.
• Jamii ya kimataifa inapaswa kulazimikia jukumu lake ili kuwazuia wazayuni wasifanye matendo mabaya hayo tena.