Uislamu na Misikiti inayo Makaburi

Swali la kumi: msimamo wa Uislamu ni nini kuhusu makaburi yanayozikwa na vipenzi wa Mwenyezi Mungu

  • | Friday, 28 August, 2015

Inayojulikana kwamba mazishi yanakuwa katika makaburi, na binadamu aliyajua makaburi hayo tangu kunguru alimfundisha mwana wa Adam muuaji kuizika maiti ya kaka yake , na mataifa yalijua namna mbalimbali kuhusu kuheshimwa baadhi ya wafu ambao wameuwawa kwa kutetea masuala ya umma, au walikuwa na heshima na nafasi maarufu kwenye umma wao au mataifa yao, na makaburi yao yaliwekwa baadhi ya alama ili yanajulikana zaidi kwa ajili ya kuyaheshima na katika wakati mwengine kwa ajili ya kuyatukana. Ama mahali pa ibada kama makanisa , miskiti n.k, inalazimisha kuwa mahali pa ibada tu sio kwa kuzika maiti, na Uislamu una shime kubwa toka mwanzo kupampanua baina ya makaburi na misikiti, kwani mafunzo yaliyotajwa katika Qurani kuhusu mataifa yaliyotangulia yanaashiria kwamba kaburi linapokuwa  msikitini inaweza kusabibisha baadhi ya matatizo, kwa sababu watu wote wanaona kwamba maiti wao ni wema wanaostahiki heshima, na maiti wa watu fulani hawi na heshima zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko maiti wa watu fulani wengeni, na kwa nini maiti yako inazikwa msikitini na maiti yangu inazikwa katika kaburi, kwa hivyo jambo hilo linasabibisha kukosekana kwa usawa baina ya maiti, na linaibua fitina na ushindani.  

Na likiwa kaburi ndani ya msikiti bila ya kizuizi, pengine itakuja zama watu hawawezi kupambanua baina ya msikiti na kaburi, na Qurani Tukufu imesema kwamba kuna baadhi ya watu ambao waliwafanya baadhi ya wema miungu, kwani watu hao walikuta picha zao "sanamu" na majina yao katika makaburi yao: {Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra.} "Surrat Nuh, aya 23", na hilo ni jinai kubwa. Na pengeni watu wanaheshimu baadhi ya wenye makaburi ilhali hawastahiki kupewa heshima hii. Na tunajua kwamba Taher Ibn AlRabia chifu wa polisi wa al-Ma'mun Khalifa wa Abbasid, ambaye amemua kaka yake Al-Amin na kuvuatana mwili wake toka Al-Rasafa hadi Al-Karkh, afisa huyo "Taher Ibn Al-Rabia" watu wamejenga msikiti juu ya kaburi lake na wameuita msikiti wa Imamu Taha katika eneo la Bab Elshekh katika Baghdad, na huyo hakukuwa ila Taher Ibn Al-Rabia chifu wa polisi wa al-Ma'mun ambaye amemua kaka yake Al-Amin.

Na tunajua pia kwamba Imamu Ali Ibn Abi Taleb kutokana na fitina alizikwa kwa siri na usiku katika Wadi Al-Ghary katika eneo la Al-najaf, na mahali pa kaburi lake hapakujulikana, lakini duru nyingi zinasema amezikwa katika Wadi Al-ghary, lakini sio mahali ambapo watu wanazuru sasa, na Imamu Fakhr El-din Al-razy mfasiri maarufu wa Qurani ambaye amekufa mwaka 606 AH ambapo amekaribia kifo amewaambia wanafunzi wake kuzikwa usiku na siri kwa kuogopa kwa iliibuliwa na Al-karamiya "ni wafuasi wa Muhammad Ibn Kram Al-Sejestani" na inajulikana kwamba alizikwa katika Huraa katika Afghanistan karibu na mlima, lakini hakuna mtu ye yote anaweza kuainisha mlima huo na kaburi lake. Na habari ni nyingi sana kuhusu jambo hilo, kwa hivyo ni lazima watu wanazikwa katika makaburi ya waislamu kutokana na Sunaa ya Mtume (S.A.W), na si kuyachukuwa makaburi kama misikiti, na pia kwa ajili ya kutojitokeza fitina mpya, kwa hivyo inapaswa kukata sehemu ya kaburi iliyopo ndani ya msikiti , na kukata uhusiana wa kaburi kwa mahai pa swala, ili kufuata aya ya Qurani inayosema { Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu. } "Surrat Al-Jen, aya 18" msikiti inapaswa kuwa msikiti , na kaburi inapaswa kuwa kaburi, na tunaweza kufanya yaliyotajwa hapo juu katika maeneo yanayoweza kuhamia makaburi kwa makaburi ya waislamu bila taabu, na kuyahamia heshima kwa makaburi ya waislamu, na msikiti unabaki msikiti kwa kumtaja Mwenyezi Mungu:  {Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni. Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka} "Surrat An-nuur, aya 36-37". Ama ikiwa kuna matatizo au fitini kuhusu kuhama kwa kaburi, basi inaweza kujenga ukuta baina ya kaburi na msikiti, na kaburi linakuwa na mlango mbali na msikiti ili watalii "wageni" wanaingia na wanatoka kupitia kwake kama iliyofanywa katika msikiti wa Sayyida Zainabu katika nchi ya Misri.
Na ilihamiwa maiti za Salman Al-Farisy na Huzaifa Ibn Alyaman maswahaba wa Mtume "S.A.W" toka makaburi yao katika nchi ya Iraq karibu na Baghdad katika miaka ya 20 karni iliyopita , na hadithi hii ni maarufu mno baina ya wanavyuoni wa Baghdad, watu wamepoogopa maji ya mto wa Dejla imefikia makaburi ya maswahaba hao na maji inaondoka miili zao mbili "R.A" iliunduwa tume ya wanavyuoni ambayo imekubali kuyachimba makaburi na kuzihamia maiti kwa makaburi mapya. na Mwenyezi Mungu anajua zaid.
Na jambo hilo ni rahisi sana kuliko kugeuka kwa fitini kutoka mara kwa mara, inatosha kutenga sehemu ya makaburi katika misikiti ambayo ina makaburi mbali na sehemu ya swala au sehemu ya Qibla kwa kizuizi kifaa cho chote, kinafanya sehemu ya swala wazi na maalumu kwa swala, na hakifanyi mtu ye yote anasema : watu wanakusali katika makaburi au wanaelekea kaburi n.k. Ama kaburi la Mtume (S.A.W) halikuwa miongoni mwa sehemu ya msikiti wakati wa amezikwa (S.A.W) kwani amezikwa mahali pa kufa kwake katika nyumba ya mama yetu Aishaa (R.A) , nyumba ambayo haiwezi kuzikwa ndani yake zaidi ya makaburi matatu, kaburi la Mtume (S.A.W) na makaburi ya maswahaba wake na makhalifa baadaye ni Abu Bakr Al-Sedeeq, na Omar Ibn Al-khatab, na kaburi la Omar AL-khatab limeachiwa na mama yetu Aishaa (R.A) ambapo yeye anatamani kuzikwa karibu na kaburi la mume wake na baba yake, na amezikwa Aisha (R.A) pamoja na mama za waumini katika Baqii Al-Ghardaq,  na Mwenyezi Mungu anajua zaid.  

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.