Hii ni Taarifa kwa Watu Majibu ya Imamu Mkuu kuhusu baadhi ya maswali yanayoulizwa katika vyombo vya habari na makongamano mengine

  • | Friday, 28 August, 2015

Mwanadamu hukua akiwa na tabia ya kupenda kujifunza, na tabia hiyo inamsukuma daima kusaka saka maarifa, kwa hiyo imesemwa kuhusu mwanadamu: "Hakika yeye hupenda kujifunza kitabia"; maana mwanadamu hupenda kujifunza na havumilii kubaki bila ya maarifa, na swali ni kifaa kimojawapo vifaa muhimu vya kuomba maarifa kwa mwanadamu akilijua vizuri, akajua vipi aliunda, alitoa kwa nani, alitoa lini, ili apate maarifa anayoyataka kutoka wajuzi katika wakati ulio mwafaka kwa kuyatoleza, wakati huo swali huwa ni sawa na kuchunguza suala la kifikira na la kisheria ambalo watu wanahitaji kubainishwa kwa haraka kwa ajili ya kukidhi haja muhimu maishani mwa jamii, kwa hiyo Uislamu umebainisha dhana ya swali na namna ya kuliunda, adabu zake na masharti yake; kwa ajili ya kuhakikisha lengo la kimafunzo.
Mwenyezi Mungu (S.W.) amewatuma manabii wabashiri na waonyaji ili wawe marejeo ya mafunzokwa wanadamu kijumla na watu wao hasa, wakijibu maswali yao, wakiwapa maarifa inayohusiana na mambo yanayoonekana na yasiyoonekana, na Mwenyezi Mungu (S.W.) hakuwaacha watu bila ya kujali kuhusu maudhui hiyo, kwa ajili ya kufikia makusudio ya waulizaji na kuwapa maarifa wanayoyataka.
Qurani takatifu ilikuwa mbele kuhakikisha jambo hilo, ambapo ilikidhi mahitaji ya waulizaji katika maudhui kadhaa, ikiainisha maswali yanayowezekana kuulizwa na yale yasiyokubaliki kuulizwa, ikafafnua tamko zake na viwango vyake, ikaelezea namna ya kutendeana nayo, na kupitia kwa mwongozo wa Qurani takatifu Mtume (S.A.W.) amewafundisha kizazi cha kwanza cha maswahaba waliokuwa wanajifunza mambo hayo, basi Qurani takatifu imetaja tamko ya "wanakuuliza", "wanakuombea fatwa" katika mara maalumu, katika tamko hizo zote tunakuta kwamba Qurani takatifu inawadokeza mwulizaji na mwenye kujibu pamoja kwa hatari na umuhimu wa njia hiyo ya kupata maarifa, Qurani inaposema: {Wanakuuliza khabarai ya miezi} Al-Baqarah: 189. Ikajibu juu ya hayo kwa kusema: {Sema: Hiyo nivipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na Hija} Al-Baqarah: 189. Hakika inaonyesha kuwa swali lililoulizwa lina baadhi ya udadisi.
Mtume (S.A.W.) amewakataa maswahaba wake akisema: "Mnitii bila ya kujadiliana nami, kwani waliowatangulieni wameangamizwa kwa sababu ya mijadala mitupu, na maswali mengi, na kutotii manabii wao"; kwa hiyo wanavyuoni wametaja aina mbali mbali za swali kwa mujibu wa kutofautiana kwa masuala husika, ambapo kuna maswali ya kujifunza na kufundisha, na swali la kukana: {Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?} Al-Baqarah: 140, na swali kukiri: {Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu?} Al-Baqarah: 106, na pia swali la kukiri na kuthibitisha mbele ya mwingine: {Wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifai mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyofichikana.} Al-Maidah: 116, vile vile kuna maswali ya kuchunguza maarifa, kama vile swali la mwalimu kwa wanafunzi wake ili ajue mafunzo na maelezo yao, na atumaini kwamba wamefahamu waliyoyafundishwa naye, na pia swali la kujifunza na kuhakikisha usahihi wa mafunzo, kama vile maswali ya wanafunzi kwa walimu wao, na watu wa kawaida kwa wanavyuoni, na kuna aina nyingine za maswali kama vile swali la kuthibitisha ujinga wa anayeulizwa, na swali la kutaka kujua maelezo maalum ya kawaida, na aina nyingine za maswali ya kutaka kujua zinazoligeuza swali likawa suala kubwa kutokana na ukweli wake, adabu zake, njia za kuliunda na kulitolea, na anayelengwa kujibu, haya yote yamelifanya suala hilo ni kama suala kubwa la kimaarifa linalokusanya mafunzo muhimu mengi anayoyasaka mwanadamu, pia kuna swali lisilo na manufaa au mafunzo yo yote, na kuna baadhi ya mambo hayaruhusiwi kuyaulizwa kwani njia za kuyajifunza hazipatikani kupitia swali peke yake, kwa sababu ya mitaala ya kujifunza yake inatofautiana na lazima kuifuatilia mitaala hiyo yote ili kupata maarifa yanayotakika. Vile vile lengo la swali lina aina nyingi, na kuna maswali yanapaswa kuundwa vyema ili kufikia jawabu lililo sawa na sahihi, na aina hii ya maswali ni yale yanayobeba sehemu ya jibu lake, ambapo mwulizaji huwa na maarifa madogo kuhusu maudhui anayoiulizia, ili amasaidie anayemwuliza kufikia jibu lililo sahihi, basi maarifa kuhusu maudhui ya swali iwe jambo la pamoja baina ya mwulizaji na anayetakiwa kujibu.
Na kila aina kati ya aina hizo za maswali ina mtindo wake, namna maalum ya kuunda kwake, maana na dhana yake, mazingira yake, wakati wa kuyauliza, na njia ya kuyauliza na kuyaunda maswali hayo inabainisha ukweli wake na inaashiria kiwango cha fikira cha mwulizaji, kwa hivyo walisema: "Swali na nusu ya Jibu", na "Swali la Kujifunza" hasa likiundwa vizuri linaainisha jambo linalotakiwa kufahamiwa kwa undani, na inabainisha lengo na kusudio lake, jambo linaloitwa na wanasheria "kuambatanisha baina ya tukio na suala", au linaloitwa na wanavyuoni wa Usuul "kubainisha tatizo", jambo linalofanya kazi ya anayetakiwa kujibu nyepesi zaidi, sawa swali hilo linahusiana na mambo ya kisiasa au kiisimu au kiuchumi au kijamii au kisheria au kifiqhi, na kwa hiyo umuhimu wa jambo linalouliziwa kwa pande zake zote utabainika.
Qurani takatifu imejaa kwa mausia na adabu na aina nyingi, zilizolifanya swali chanzo kikubwa cha kupata maarifa lisilofai kupuuzwa na mwanafunzi, ambapo kuuliza na kutoa maswali ni dalili ya kutaka kupata maarifa, na katika wakati huo huo jambo lisilomalizika maishani yote, basi swali likimalizika uhai huisha, na mwanadamu anayeuliza uliza hutambuliwa kama ana uhai kamili, akikataa kuuliza huwa ni kama maiti isiyo na uhai, na swali ni njia ya kupata maarifa kuhusu mambo mengi, ambapo mambo yanayotoka nje ya mazingira ya kuyauliziwa na machache sana yakiwemo mambo yanayojulikana kwa dharura kiakili yasiyohitaji kuthibitishwa kwa dalili.
Kuuliza kulikuja katika Qurani takatifu katika maudhui tofauti na kwa njia mbali mbali na kwa malengo mbali mbali, na kila swali lilikuwa na hekima na hukumu yake, Imamu Bin Al-Atheer –M.M. amrehemu – amesema: "swali katika kitabu cha M.M. na sunnah ya Mtume (S.A.W.) limekuja katika aina mbili: ya kwanza: lililokuja kwa ajili ya kubainisha na kujifunza kwa mambo ya dharura, basi aina hiyo ama ni mubaha au ni afadhali kuulizwa au ni lazima liulizwe, ambapo mwanadamu akiyauliza mambo hayo basi hamna neno:
"pia, kuna swali linalolengea kupata elimu na maarifa; na aina hii inagawanyika katika mafungu mawili: la kwanza ni lile swali lililo na jibu kwa urahisi, na la pili ni lile swali lisilo na jibu kwa urahisi kwa sababu ya kutokuwepo maarifa ya lazima ya kujibu swali hilo maana jibu lake ni gumu sana kiakili au inawezekana kuwa kuficha jibu ni afadhali zaidi kuliko kulifichua.
Kati ya maswali yaliyokuja kwa kuomba elimu ya ziada na majibu yake yametajwa katika Qurani na Mwenyezi Mungu hakuwakataza manabii kuyauliza, kauli yake (S.W.) kupitia nabii wake Ibrahim (A.S.): {Na alipo sema Ibrahim: Mola wangu Mlezi!Nionyeshe vipi unavyo fufua wafu. Mwenyezi Munguakasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ilimoyo wangu utue. Akamwambia: Twaa ndege wanne nauwazoeshe kwako, kisha uweke juu ya kila kilima sehemu, kisha wete, watakujia mbio. Na ujuekwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu,na Mwenye hikima.} Al-Baqarah: 260. Na kauli yake (S.W.) kupitia nabii wake Mussa (A.S.) {Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Molawake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi!Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahalapake basi utaniona. Basi alipo jionyesha Mola Mleziwake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema:Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wakwanza wa Waumini} Al-Araaf: 143, ambapo swali hilo halikataliwi na Mwenyezi Mungu (S.W.) juu ya Mussa (A.S.) lakini alifungamana baina ya kutoa jibu lake na kutulia kwa mlima wakati wa kumwona Mwenyezi Mungu, na hayo kwa kuwa udhaifu wa binadamu mbele ya kumtazama Mwenyezi Mungu, na katika hali mbili Mwenyezi Mungu hakukataa swali la nabii wake Ibrahim au nabii wake Mussa kwani lengo la swali hilo ni kuomba elimu ya ziada na maarifa.
Na kuna aina nyingine ya maswali yatolewayo kwa ajili ya kujifunza lakini hayakuwa na majibu kwa hekima za Mwenyezi Mungu, kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu} Al-Israa: 85, ambapo kuficha siri ya roho ili kubainisha udhaifu wa binadamu kutambua ukweli wa nafsi yake basi udhaifu wake kutambua muumbaji utakuwa jambo la kawaida, na hekima ya hayo kubainisha kasoro ya akili kutambua kiumbe kinachofanana nayo jambo linalomaanisha kwamba hawezi kutambua muumbaji wake, na ili kudokeza kwamba swali hilo kuhusu suala linalohusiana na mambo yasiyoonekana ambapo muulizaji haruhusiwi kuliulizia, bali anapaswa kujua kwamba elimu yake haimpe nafasi ya kutambua kila kitu. Na kauli yake (S.W.): {Wanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haikujiini ila kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini aghlabu ya watu hawajui} Al-Araaf: 187, na swali likitolewa na mayahudi au washirikina wa Makkah lakini miadi ya siku ya kiyama imefichika ili mwanadamu awe na tahaddhari wakati wote. Na kati ya maswali yaliyo magumu kabisa kama vile: alikuja mtu kwa iamamu Malik akasema: Ewe Malik! Arrahmani, Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu ya Kiti cha Enzi, vipi ametawala? Imamub Malik akajibu: "kutawala kwake ni jambo lajulikanalo, na namna isijulikanayo, kuuamini ni wajibu, kuuliza juu yake ni bida'a. Kisha akasema: na sikukuona ila mwenye bida'a".
Vile vile kuna swali linalosababisha madhara, na jibu lake liwe na mashaka zaidi, wakati huo swali hilo linazingatiwa miongoni mwa maswali yanayokataliwa, mfano wa maswali hayo ni yaliyotajwa katika kauli yake (S.W.): {Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole} Al-Maidah: 101, na hakika mkiyauliza maswali hayo – mkidhani kwamba mnasababisha mashaka na mateso kwa anayetakiwa kujibu na mnadhihirisha dosari wake na uchache wa elimu yake – basi kwa kweli Qurani mtukufu inaweza kuyaonyesha kwenu itakapoteremshiwa, lakini hakika majibu ya maswali hayo hayana manufaa kwenu kwani yanazingatiwa maarifa yasiyo na faida. Mambo hayo ni madogo kwa mambo menigineo, na aghalabu ya maswali ya aina hii yametajwa katika maudhui zisizohusiana na makalifisho ya Mwenyezi Mungu (S.W.), kama vile maswali yaliyohusiana na ng'ombe wa Banu Israel.
Na kuna maswali ya kudhihirisha dosari na ya kufanya mzaha na dhihaka kama katika kauli yake (S.W.): {Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshia kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi kwa hiyo dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumuabudu, baada ya kwisha wajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa nguvu zilizo dhaahiri} Al-Nisaa: 153, na kauli yake (S.W.): {Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii. Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyo dai; au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso. Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na Mtume?} Al-Israa: 90-93, au kufanya kejeli kama vile kauli yake (S.W.): {Na walipo sema: Ee Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ni kweli itokayo kwako basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo chungu} Al-Anfaal: 32.
Licha ya maswali yaliyokuja katika Qurani Mtukufu kuhusu ulimwengu na ugunduzi wake na shime kubwa iliyopewa na Qurani kwa jambo hilo, Mwenyezi Mungu amesema: {Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?} Al-Ghashiya: 17-20, na kauli yake (S.W.) {Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi} Al-Nisaa: 82, na kauli yake: {Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?} Adh-dhariyaat: 21.
Basi maswali ni chanzo muhimu cha kuomba elimu na maarifa yo yote na ugunduzi mpya ulimwenguni, ambapo ugunduzi wa ndege haufikiliwi ila baada ya kuchunguza viumbe vingine vinavyoweza kuruka, na kuuliza kuhusu namna ya kumfanya mtu aweza kuruka, na kivutio hakijulikana ila baada ya kutolewa swali na Nyutin kuhusu sababu ya kuanguka tufaha kutoka juu hadi chini, na umeme haujuliwi ila baada ya kuchunguza jua na nyota na kutafuta njia nyingine ya kupata mwangaza kwa binadamu zikizimwa …, na kadhalika.
Basi ni wito ya dharura ya kusisitiza umuhimu wa kutoa maswali. Mbona mwanachuoni huyu alipendelea mtazamo huu sio mwingine? Na nini dalili zake? Na nini kiwango cha usahihi wa dalili zake? Mbona nafuata mwelekeo huu wa kisiasa hasa? Ni nini sababu na malengo? Mbona mimi ni mwislamu na sio mfuasi wa dini nyingine? {Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina} Yossuf: 108, basi ulinganiaji kwa Mwenyezi Mungu lazima uwe na dalili thabiti (hoja), na hali kadhalika wakati wa kufuata wito maalum (lazima uwe na hoja) ili uweze kukabiliana na changamoto zo zote, na jambo hilo haliwezekana kutekelezwa kupitia kuiga tu kwani hiyo ikikubalika makafiri huweza kudai kwamba wanaiga tu basi hawakuwa na adhabu.
Adabu ya Swali:   
  Anayetakiwa kujibu swali ana haki kuzungumza na muulizaji ili amsaidie kueleza kusudio lake; ili aweze kujibu swali lake, na muulizaji ana haki kuomba maelezo zaidi baadaye ili ajitumaini kwamba amepata jibu lililo sawa; kwani kuna baadhi ya majibu yasiyotosha mahitaji ya muulizaji, na kiwango cha maswali yakiwa magumu na yenye maelezo mengi majibu pia yanakuwa na kiwango hicho hicho, na hayo yote yanabainisha maendeleo ya kimawazo na kitamaduni ya jamii husika (ya muulizaji na anayetakiwa kujibu), na watu wa umma kijumla.
Na kati ya alama za kupotoka kutolea maswali yenye kiwango cha chini, au yanayohusiana na mambo yasiyo na manufaa, na mwanachuoni anapaswa kuwafundisha wanaojifunza namna ya kuendeleza kiwango cha maswali yao: {Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole} Al-Maidah: 101, na awafundisha watu kwa upole kuhusu namna ya kuuliza na wakati wa kuuliza.
Na katika zama za fitina muulizaji na anayetakiwa kujibu wana wajibu wa kumcha Mwenyezi Mungu katika swali na jibu lake, na lazima wajiepushe na maswali na majibu yanayosababisha kueneza fitina, na kukuza chuki, na kupelekea migogoro ya ziada, kwani neno ni jukumu kubwa, hasa likiambatanishwa na fitina, basi ni lazima waulizaji wamche Mwenyezi Mungu, na wanaotakiwa kujibu pia, hakika Mwenyezi Mungu (S.W.) atamwuliza kila mtu juu ya kazi yake, na kauli ya mtu ikiwa swali au jibu ni sehemu kati ya kazi yake, na kwa kweli kila mja atahesabiwa mbele ya Mwenyezi Mungu (S.W.) kuhusu maswali yake na majibu yake, ambapo ni sehemu mojawapo amali zake zilizoandikwa: {na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha} Yassiin: 12.
Na mataifa yasiyouliza, au hayajui namna ya kuyaunda maswali yake, hayajui mambo ya dharura yake, na hayatambui hatima zake. Baadhi ya mahujjaji waliotoka nchini Iraki wamekwenda Hijja, baadhi ya watu wameashiria Abdullah Bin Umar mmoja wa maswahaba wa Mtume (S.A.W.) na mwana wa rafiki yake, na mmoja wa maswahaba wakubwa wenye kujua kusoma Qurani – wakamjia wakimuuliza kuhusu baadhi ya mambo ya dini yao!! Akawajia, wakamwuliza juu ya damu ya kiroboto; anaweza mmoja kusali akivaa nguo zilizopatwa na damu hiyo? Basi yule swahabi (R.A.) akaonyesha ghadhabu akisema: "Je, mwana wa binti ya Mtume (S.A.W.) ameuawa ardhini mwenu na hamkuuliza kuhusu hukumu ya damu yake, bali mnauliza kuhusu hukumu ya damu ya kiroboto?". Umma unapokuwa katika hali duni hii, basi hakuna suluhisho ila kuboresha au kubadilisha, Na jambo hilo likitolewa na wakubwa wa watu - wano elimu na ujuzi- sio watu wa kawaida tu basi hapo ndipo janga na tatizo kubwa zaidi.
Na kwa upande wa maswali ya kifiqhi na mikutano yake na kongamano zake hatukuona miongoni mwa maswali yanayotolewa yale yanayohusiana na maudhui ya "Umoja wa Umma" hasa kuhusu changamoto na vikwazo, pia hatukuona maswali yanayohusiana na migodi ya madini yaliyomo ardhini, je umiliki wake ni wa wanaoishi ardhini ile au ni wa umma?! Na namna ya kuzitumia pesa na masharti yake, na msimamo wa umma na sheria kuhusu jambo hilo, Abu Al-Alaa Al-Muariy amekosa aliposema kwa jogoo mdogo: "wamekudharau wakakupa sifa duni, je wanaweza kufanya hivyo na mwana wa samba"?!
Na kati ya maswali yale yanayokusudiwa kuonyesha dosari au aibu au kiburi….!
Basi wanaozingatia dini yao, wanaotaka kujifunza mambo ya dini na kupata maarifa kuhusu fiqhi wanapaswa kumcha Mwenyezi Mungu (S.W.) katika maswali yao katika uwanja wo wote, na watilie mkazo adabu ya kuuliza maswali na masharti yake, ambapo mtu anayejua kwamba majibu ya maswali yake -yakienezwa kwa watu wa kawaida- yatasababisha kuzuka fitina, basi ni afadhali ajiepushe na maswali ya namna hii kabisa.
Matukio ya hivi karibuni pengine ni funzo muhuimu linalowapa maulamaa na wasomi wetu jukumu la ziada pamoja na majukumu yao mengi, nalo ni jukumu la kuwafundisha watu namna ya kuuliza na adabu zake, kisha kuwafundisha na kuwaelimisha mambo yanayowanufaisha katika nafsi zao na jamii zao hapa dunia na akhera, kwa ajili ya kujiepusha na maneno matupu na maswali mengi yasiyo na faida yanayoweza kusababisha migongano ambayo umma hauistahmili zaidi, na inawezekana msemaji mmoja atamka neno moja bila ya kujali, hatimaye huangamizwa motoni kwa sababu ya neno hilo.
Sisi tunasisitiza udharura wa kufahamu utangulizi huu wakati wa kuyaunda maswali ili kuwauliza mwanachuoni, au mwenye kutoa fatwa, au msomi wa fiqhi yule au huyu, ambapo utangulizi huu ni muhimu sana ili kuwasaidia wote wafahamu roli muhimu ya swali ya kupata maarifa, na imekuja wakati wa kujibu kundi la maswali ambayo yameainishwa kupitia mazoezi ya kuangalia ambapo ni maswali yanayoulizwa mara kwa mara kwa sababu tofauti, na tumejaribu kutoa majibu yanayoweza kutosheleza mahitaji ya muulizaji, wakati huo huo yanafaa kuwa mfano mzuri wa kuyaunda maswali na kutoa majibu yake, tunasema kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na mafanikio yake:

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.