Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu Shirika la Kimataifa la Msamaha (Amnesty)

  • | Wednesday, 12 August, 2015
Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu Shirika la Kimataifa la Msamaha (Amnesty)

-    Al-Azhar Al-Shareif yalaani wito wa shirika la kimataifa la msamaha (Amnesty) wa kutozingatia ukahaba ni jinai….ikisistiza:
-    Wito hii ni ukiukaji wa heshima ya mtu na kumfanya mtumwa na mwili wake
-    Uislamu umeainisha uhusiano wa kijinsia katika ndoa inayohalalishwa kwa mujibu wa maksharti hasa ya dini ya haki  

Al-Azhar Al-Shareif inalaani wito mbaya uliotolewa na shirika la kimataifa la msamaha (Amnesty), wakati wa mkutano wake wa mara kwa mara uliofanyika tarehe 7-11 mwezi wa Agosti unaoendelea, ambapo shirika hilo limeombea kutozingatia ukahaba ni jinai inayostahiki adhabu.

Na Al-Azhar inasisitiza kwamba wito hiyo ambayo inakuja katika mfululizo wa majaribio maovu makali ya kuharibu maadili, ni ukiukaji wa heshima ya mtu ambaye alipewa heshima kubwa na Mwenyezi Mungu akimpendeleza juu ya viumbe vyake vyote, na uvunjaji wa maumbile yake aliyoumbwa nayo, pia ni njia ya kumgeuza mtu akawa mtumwa na kuhalalisha kuufanyia biashara mwili wake, na uharibifu wa haki zake alizozipewa na Mwenyezi Mungu na zilizopitishwa na sheria za mbinguni zikiongozwa na dini ya kweli ya Uislamu.

Vile vile Al-Azhar Al-Shareif inasisitiza kuwa Uislamu uliainisha uhusiano wa kijinsia kwa ndoa sahihi iliyohalalishwa katika sheria kwa masharti yaliyofaradhishwa na dini ya haki ambayo iliainisha nguzo zake na masharti yake ya lazima, ili iwe ndoa hiyo ya mapenzi na kuruma sio kwa kukidhi ladha ya wakati maalum tu, ikaharamisha husiano mbaya nyinginezo zote zilizo kinyume na ndoa, kwa ajili ya kuuhifadhi utu kutoka shari ya kuanguka katika machafuko ya uzinzi na uhuni na uchafushaji wa kijamii na wa kifamiliya.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.